The House of Favourite Newspapers

Vodacom Yatangaza Taarifa Ya Mwaka Unaoishia Machi 31, 2023, Yaonyesha Kuimarika Kifaida

0
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Bw. Philip Besiimire

Dares Salaam – Mei 12, 2023.Kampuni pekee ya mawasiliano ya simu iliyoorodheshwa kwenye soko la hisa la Dar es Salaam, Vodacom Tanzania Plc, imetangaza taarifa ya ripoti ya awali ya miezi 12 iliyopita inayoishia mwezi Machi 31, 2023 ambayo inaonyesha ukuaji mkubwa kwa kuzalisha shilingi trilioni 1.1 za mapato ya huduma.

Akizungumza na wawekezaji Pamoja na wadau wengine wa kampuni kwa njia ya simu wakati wa kutangaza matokeo ya awali ya ripoti hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Bw. Philip Besiimire ameelezea kuwa ripoti imeonyesha kuimarika kwa faida kwa mwaka uliopita ambapo imechochewa na kampuni kutimiza adhma yake ya kuwahudumia wateja pamoja na shughuli mbalimbali za kunufaisha jamii ya watanzania nchini kote.

“Ni Fahari kwamba tumepiga hatua kwa mwaka uliopita huku tukiwa tumetekeleza adhma ya kuwahudumia wateja wetu kadri ya mikakati tuliyojiwekea. Pia, imetutia moyo kuona namna tulivyofanikisha miradi mbalimbali ya shughuli za kijamii pamoja na kujiendesha kwa faida,” alisema Philip.

Vodacom imeonyesha kupata faida ya shilingi bilioni 44.6 baada ya kodi, ni hatua kubwa ukilinganisha na hasara ya shilingi bilioni 20.3 kwa mwaka uliopita. Ukuaji huu umechochewa na ongezeko la matumizi ya intaneti, kuimarikakwa M-Pesa, ongezeko la ukuaji katika pato la kudumu ambalo ni ongezeko mara mbili mwaka-kwa-mwaka, na kuzalisha faida ya kuridhisha kwenye mapato ya huduma.

Mapato ya kupiga simu yamepungua kwa 1.2% na kufikia shilingi bilioni 283.5, ikionyesha ushindani mkubwa kwenye bei.

Hata hivyo, mapato ya M-Pesa yamekua kwa 8.4%  na kufikia shilingi bilioni 357.1 yaliyotokana na matumizi ya huduma mpya na mbalimbali. Mapato ya matumizi ya intaneti yameongezeka kwa 34.2% na kufikia shilingi bilioni 273.7, na kuonyesha uhitaji mkubwa wa matumizi ya huduma za intaneti pamoja na ukuaji wa simu janja. Ukuaji wa pato la kudumu umeongezekakwa 27.3% na kufikia shilingi bilioni 19.5, lililotokana na uwekezaji katika miundombinu na ongezeko la wateja wapya.

Kwa upande mwingine, mapato kabla ya riba, kodi, kushuka kwa thamani na upunguzaji wa madeni yameongezeka kwa 9.7% nakufikia shilingi bilioni 329.4, ikiwa imechochewa na ukuaji wa kiasi kikubwa na ufanisi kwenye kudhibiti matumizi. Kampuni imeonyesha uthabiti licha ya changamoto mbalimbali za kiuendeshaji zinazoendelea duniani, kufanikisha kudhibiti gharama za uendeshaji.

Vodacom Tanzania imepiga hatua kubwa kwenye utekelezaji wa miradi ya kijamii, kwa kutumia fursa ya teknolojia kuboresha maisha na maendeleo na manufaa mapana. “tumeongeza usajili wa wakulima kwenye huduma yetu ya M-Kulima na kufikia milioni 3.1 kutoka 140,000 ambao walisajiliwa mwezi Machi 2022.

Kupitia M-Pesa, jumla ya shilingi bilioni 4.6 ziligawanywa kwa wakulima ambao walijiunga, kutoa usalama na ufanisi wa miamala ya kifedha, taarifa za masoko, na utabiri wa hali ya hewa,” alisema Philip.

Pia kampuni ilijikita katika mpango wake wa ‘ujumuishi kwenye kujali,’ uliolenga kuwezesha mazingira rafiki ya kutoa huduma kwa watu wenye mahitaji maalum. Madawati maalum ya kutolea huduma katika maduka yalianzishwa na kutekeleza huduma ya kutumia lugha ya alama kwa njiaya video kwenye mtandao wa WhatsApp. Zaidi ya wateja 1,300 walinufaika kutokana na mpango kwa kipindi cha mwaka wa jana wa fedha.

Pia, mwaka 2022 Vodacom ilizindua mtandao wa huduma ya 5G kwa mara ya kwanza nchini ikiwa ni utekelezaji wa dhamira ya kampuni ya kuipeleka Tanzania kwenye zama za kidigitali kupitia mikakati endelevu.

Hili limeenda sambamba na uwekezaji wa kampuni katika mtandao wake ili kufikia ukuaji wa mahitaji ya wateja ambapo shilingi bilioni 156.0 zilielekezwa kwenye kusambaza huduma za mtandao, kuongeza ufanisi, na miundombinu ya teknolojiaya Habari kwa kuongeza minara 390 ya mawasiliano ya 4G, minara 231 ya 5G, na kutandaza kilometa 283 za mfumo wa faiba ambao ni muhimu katika kuongeza matumizi ya 4G na 5G, vilevile kuwapatia wafanyabiashara mtandao wenye kasi yenye ubora wa hali ya juu.

“Kupanda kwa huduma za kimkataba kwa kila mwaka, hususani zinazohusisha kukodisha minara, na uwekezaji wa ziada katika uvumbuzi wa teknolojia kama vile 5G ulichangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa gharama za uendeshaji kwa mwakahuu.

Kwa kuongezea, tuliwekeza Dola za Kimarekani milioni 63.2 katika mnada wa wigo unaotolewa na Mamlama ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kufanikiwa kununua masafa manne muhimu ya wigo wa chini na wakati wa mawasiliano ya matandao wa 5G.

Kwa uwekezaji huu, tutaweza kuongeza ukuaji na uwezo wa ufikiaji wa kudumu na kuwezesha kufanikisha kupunguza mgawanyo usio sawa wa matumizi ya kidigitali uliopo sasa,” alisema Philip.

M-Pesa imeonyesha mwenendo wa  ukuaji ambao umesababishwa na kupunguzwa kwa tozo za serikali kwenye huduma za pesa kwenye simu za mkononi na mkakati wa kampuni na upanuzi wa huduma tofauti za kifedha kwenye mtandao wake.

“Kutokana na kupunguzwa kwa tozo za serikali, kiasi cha miamala baina ya mtu-na-mtu na kutoa pesa kinaongezeka.

Tunatoa rai kwa serikali kuendelea kupunguza kodi, kwani kumepelekea kuimarika kwa huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi na kupelekea kuunga mkono nafasi ya M-Pesa kwenye ujumuishi wa huduma za kifedha. Tumefanikiwa kuongeza idadi ya makampuni yaliyojiunga mfumo wetu wa malipo kwanjia ya kielektroniki, kwa kukua kwa kiasi kubwa na kufikia 150,000.

Miamala ya zaidi ya shilingi trilioni 6 ilifanywa kidigitali na wateja milioni 2 kupitia wafanyabiashara wetu. Kwa kuongezea, huduma za kukopa za Vodacom ziliwahudumia wateja zaidi ya milioni 4, ambapo shilingi trilioni 1 za mikopo midogomidogo, ikiwemo msaada wa kifedha wa muda mfupi kwa mawakala 75,000,” aliongezea Philip.

“Tutaendelea kuwekeza katika miundombinu ya mtandao wetu ili kuwapatia wateja bidhaa na huduma zenye ubora wa hali ya juu pamoja na ubunifu kwenye bidhaa za M-Pesa na kuchangia kufikia ujumuishi kwenye huduma za kifedha na kidigitali.

Kama kampuni inayowajibika, Vodacom itaendelea kushirikiana na serikali katika masuala yote yahusuyo biashara na kuendeleza mahusiano mazuri,” alihitimisha Philip.

Leave A Reply