The House of Favourite Newspapers

Vodacom Yawakabidhi Pikipiki Zao na Bajaj Washindi wa Twende Mjini na M-Pesa

0
Mgeni rasmi ambaye ni Afisa Tarafa wa Kinondoni, Rahma Kondo katikati akizungumza kwenye hafla hiyo, kushoto ni Mkuu wa Maendeleo ya Biashara ya M-Pesa, Tulisindo Rashid na kulia ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya Dar es Salaam na Pwani.

KAMPUNI ya Mawasiliano ya Vodacom PLC imewakabidhi wateja wake zawadi walizojishindia kwenye Promosheni ya TWENDE MJINI ambayo kila siku anapatikana mshindi mmoja wa pikipiki mpya aina ya Boxer na kila wiki anapatikana mshindi wa Bajaj mpya aina ya TVS ambapo wiki ya nane itakapokuwa ikielekea ukingoni itatolewa gari mpya ya kisasa aina ya Corola Cross.

Mkali wa Singeli Dullah Makabila akifanya yake wakati mambo yakiendelea.

Washindi hao wamekabidhiwa zawadi hizo kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Bunju A, Dar eneo ambalo ametokea mshindi wa Bajaji ambapo katika kuwakabidhi zawadi hizo kulikuwa na burudani ya muziki kutoka kwa mkali wa singeli, Dullah Makabila.

Washindi hao walikabidhiwa zawadi hizo na Katibu Tarafa wa Kinondoni, Rahma Kondo aliyemuwakilisha Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Stellah Msoffe.

James Pili Joseph kushoto akipokea funguo ya pikipiki aliyojishindia.

Akizungumza kwenye hafla ya utoaji wa zawadi hizo, Mkuu wa Kanda wa Vodacom Kanda ya Dar es Salaam na Pwani Brigita Stephen aliwapongeza washindi hao kwa ushindi na kuwasihi kuendelea kutumia huduma za M-Pesa ili waendelee kushiriki na kuweza kujishindia tena.

Washindi wakiwa kwenye pikipiki zao baada ya kukabidhiwa.

Brigita amesema vigezo vya kuweza kushinda zawadi hizo ni kutumia mtandao wa Vodacom na kufanya mihamala kupitia M-Pesa kwa kubonyeza *150*00# au kuingia kwenye App ya M-Pesa ndipo unapokuwa umeingia kwenye bahati nasibu hiyo, alisema.

Balozi wa Vodacom mchekeshaji, Idris Sultan na Katibu Tarafa wakimkabidhi mfano wa funguo mshindi wa Bajaj, Nyanjige Paul (katikati) kulia ni mtangazaji Salama Jabir ambaye naye ni balozi wa Vodacom.

Waliokabidhiwa zawadi zao kwenye hafla hiyo ni James Pili Joseph, Ramadhani Mponda aliyewakilishwa na Doris Jeremiah na Francis Kiwale hawa wote wamekabidhiwa pikipiki walizoshinda.

Nyanjige akipewa mkono wa pongezi sambamba na ufunguo halisi wa Bajaj aliyoshinda.

Hao wakiondoa na pikipiki mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anayesoma mwaka wa mwisho amekabidhiwa Bajaj aliyoshinda.

Washindi hao walikabidhiwa zawadi hizo na Katibu Tarafa Rahma Kondo pamoja na mabalozi wa Vodacom, msanii wa vichekesho, Idris Sultan na Mtangazaji Salama Jabir.

Nyanjige akiwa kwenye pozi la furaha katikati ya mama zake.

Naye Mkuu wa Maendeleo ya Biashara za M-Pesa, Tulisindo Rashid amewaasa wananchi wote kutumia huduma za M-Pesa kufanya muhamala wowote unaweza kujishindia zawadi kama hizo.                                                                                                                                                  HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply