The House of Favourite Newspapers

Vongozi wa Qatar na Misri wakutana kujadili mikakati ya kumaliza mgogoro wa Israel na Hamas

0
Kiongozi wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani alipokutana na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi mjini Cairo, Misri Juni 24, 2022.

Viongozi wa Qatar na Misri wamekutana mjini Cairo siku ya Ijumaa, wote wakiwa na matumaini ya kupatanisha kuondoa hali hiyo ya ghasia huko Ukanda wa Gaza, upelekaji wa misaada ya kibinadamu na kuachiliwa kwa mateka wa Israel.

Mazungumzo kati ya Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi na Emir Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani walijadili juhudi madhubuti za kufaikishia sitisho la mapigano huko Gaza na usambazaji wa misaada ya kutosha kwa wakazi wake milioni 2.3 waliozingirwa, taarifa kutoka ofisi ya Sisi ilisema.

Qatar ilisema “juhudi za pamoja za kukomesha uchokozi dhidi ya Gaza, kupunguza mapigano na upelekaji misaada ya haraka ya kibinadamu” zilijadiliwa.

Ziara ya amir wa Qatar inakuja siku moja baada ya waziri mkuu wa Qatar kukutana na wakuu wa Shirika la Kijasusi la Marekani (CIA) na Shirika la Kijasusi la Israel Mossad mjini Doha kujadili vigezo vya mpango wa kuachiliwa kwa mateka na kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas.

Rais wa Marekani Joe Biden akiwa na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi, Amiri wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani; na Mwanamfalme wa Kuwait Meshal al-Ahmad al-Jaber al-Sabah huko Saudi Arabia Julai 16, 2022.

Qatar, ambako viongozi kadhaa wa kisiasa wa Hamas wanaishi, imekuwa ikiongoza upatanishi kati ya kundi la wanamgambo wa Palestina na maafisa wa Israel kwa kuachiliwa kwa zaidi ya mateka 240 waliochukuliwa na wapiganaji wa Hamas Oktoba 7, katika shambulio ambalo Israel inasema watu 1,400 waliuawa.

Tangu wakati huo Israel imeanzisha mashambulizi yasyosita na uvamizi wa kivita katika eneo la Gaza linaloongozwa na Hamas, ambapo zaidi ya watu 10,000 wameuawa, kulingana na maasifa wa Palestina.

Misri pia imekuwa ikifanya mawasiliano na Hamas pamoja na Israel na imekuwa ikishiriki katika mazungumzo, ikiwa ni pamoja na utoaji wa misaada kupitia mpaka wake wa Rafah na Gaza na uhamishaji wa watu kutoka eneo la watu wenye pasipoti za kigeni na baadhi Wapalestina wanaohitaji matibabu ya haraka.

Umoja wa Mataifa umesema malori 65 ya misaada yaliingia Gaza kutoka Misri siku ya Alhamisi, chini ya idadi inayohitajika katika kushughulikia ongezeko kwa mgogoro wa kibinadamu.

TAKUKURU YANUSA HARUFU ya RUSHWA UKUSANYAJI KODI ya ZUIO….

Leave A Reply