The House of Favourite Newspapers

Wabunge Kuchukua Likizo Kurekodi ‘Jerusalema’

0

WABUNGE nchini Kenya wiki ijayo watachukua mapumziko mafupi kwenda kurekodi video ya densi ya Jerusalema maarufu kama #JerusalemaDanceChallenge ambayo imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii.

 

Wimbo wa Jerusalema ulioimbwa na mwanamuziki wa Afrika Kusini, Master KG, umechochea kutengenezwa kwa video nyingi kote duniani.

 

Kiongozi wa walio wengi wa bunge la Kenya, Amos Kimunya, amenukuliwa akisema spika na wakuu wote wa kamati za idara mbalimbali wataongoza wabunge wengine katika densi hiyo.

 

Alisema video hiyo itaangazia kazi za bunge na kuonyesha umoja na waathirika wa janga la virusi vya corona.   Jennifer Shamalla, mbunge maalum, ametuma video kwenye mtandao wa Twitter inayoonyesha wabunge wenzake wakifanya mazoezi.

Leave A Reply