The House of Favourite Newspapers

WACHACHE WAJITOKEZA MARUDIO UCHAGUZI WA UDIWANI MBWENI, DAR

0
Mawakala na wasimamizi wa kura wakiwa wametulia kwenye viti wakisubiri wapiga kura ambao walifika kwa idadi ndogo.
Zoezi la kupiga kura likiendelea, ambapo wasimamizi wakijaza taarifa za mpiga kura (hayupo pichani)
Msimamizi wa kituo cha kupiga kura akihakiki jina la mpiga kura kwenye daftari la kudumu la kupiga kura.

 

UCHAGUZI  wa  marudio ya  udiwani  katika  kata 43 unaofanyika leo sehemu mbalimbali nchini,  umeleta  hali  ya  sintofahamu katika Kata ya Mbweni jijini Dar es Salaam ambako wapiga kura wamejitokeza kwa idadi ndogo kuliko ilivyotegemewa.

 

Global  TV  Imefanikiwa  kufika Kata ya Mbweni, wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam na  kutembelea baadhi  ya  vituo hivyo ambapo pamoja na hali hiyo, imebaini  usalama wa  kutosha   ambako mawakala na  wasimamizi walionekana katika hali ya  kuchoka na wengine kupitiwa na usingizi.

 

Uchunguzi uliofanywa unaonyesha hali hiyo ilitokana na kusubiri wapiga kura  ambao  walikuwa wakifika hapo mmoja-mmoja  baada ya muda mrefu.

 

Kwa mujibu wa takwimu,  idadi  ya  wapiga kura waliokuwa  wakitegemewa  kwenye kata ya  Mbweni ni  zaidi  ya  400 lakini mpaka Global TV inaondoka hapo mchana huu, ni   wapiga  kura  24 tu waliokuwa wamefika hapo.

 

NA CATHERINE KAHABI/GPL

Leave A Reply