The House of Favourite Newspapers

Viongozi Wadai: Maghorofa ya Mbunge Yageuzwa Chaka la Wakabaji!

0

sh amonSauli Henry Amon.

Richard Bukos na Issa Mnally, UWAZI

Dar es Salaam: Majengo ya ghorofa zaidi ya sita ambayo hayajaendelezwa ya Mbunge wa Rungwe mkoani Mbeya kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sauli Henry Amon (pichani) ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya S.H Amon, yanalalamikiwa kwa kufuga vibaka ambapo wananchi wamelalamika na kutaka polisi kuingilia kati.

Vyanzo vyetu vya kuaminika vilidai kuwa majengo hayo yapo maeneo ya Tabata-Mawenzi jijini Dar ambayo kwa sasa ni tishio kwa wapita njia hasa majira ya jioni ambapo mara kadhaa pameripotiwa kutokea vitendo vya uhalifu wa ukabaji na uporaji.

maghorofa ya mbunge (1)Maghorofa yaliyogeuzwa vichaka.

Kufuatia malalamiko hayo, hivi karibuni, wanahabari wetu walifika eneo hilo na kujionea majengo hayo yaliyozingirwa na vichaka vikubwa huku vijana kadhaa ambao shughuli yao haikufahamika wakionekana kurandaranda maeneo hayo.

Wakiwa kazini maeneo hayo, wanahabari wetu walikumbana na vibaka waliotaka kuwapora vitendea kazi vyao lakini kutokana na mbinu za waandishi wetu, juhudi zao ziligonga mwamba.

MAGHOROFA (1)Mwenyekiti wa Mtaa

Baada ya kutoka kwenye maghorofa hayo yanayodaiwa kutelekezwa na mbunge huyo, gazeti hili lilifika kwenye Ofisi za Serikali ya Mtaa wa Amani Kata ya Tabata-Mawenzi, Dar na kumkuta Makamu Mwenyekiti wa mtaa huo, Samwel Mbwambo ambaye alikiri majengo hayo kuwa kero kwenye mtaa wake.

“Ndugu waandishi, hili eneo limekuwa kero kubwa kwa sababu tumechoka kupokea taarifa za uhuni ikiwemo ukabaji vinavyofanyika kwenye eneo la majengo hayo.

maghorofa ya mbunge (4)Maghorofa yaliyogeuzwa vichaka.

“Majengo hayo yamechukua eneo kubwa hivyo eneo lote limekuwa hatarishi, hali iliyosababisha ofisi yangu iongeze ulinzi.

“Eneo hilo mwanzo lilikuwa likimilikuwa na Tanzania Elimu Supplies (TES), walikuwa wakitaka kujenga nyumba za wafanyakazi wao lakini baadaye walisimamisha ujenzi kisha kumuuzia S.H Amon (mbunge huyo).

“Baada ya S.H Amon kulinunua, alikwenda Wizara ya Ardhi kuangalia ramani ya eneo lake, akagundua kuna wakazi wamejenga kwenye eneo lake hivyo akafungua kesi kudai eneo lake lililomegwa.

 MAGHOROFA (2)“Wakati kesi hiyo ikiendelea, mahakama ilizuia ujenzi wa aina yoyote kwa wakazi wanaodaiwa kuingia eneo lake pamoja na yeye mwenyewe. Ndiyo maana eneo hilo limekuwa chaka la vibaka,” alisema kiongozi huyo.

Gazeti hili lilipomtafuta mbunge huyo na kumuuliza juu ya kutelekeza majengo hayo na kwamba yanafuga vibaka, alisema hajayatelekeza ndiyo maana kuna jengo moja ambalo limepakwa rangi.

Kuhusu kufuga vibaka, Amon alihoji: “Kwani hao vibaka wanafanya vitendo hivyo saa ngapi?

Uwazi: Ni muda wote kwani hata sisi (waandishi tumefika na kunusurika kuporwa muda wa saa 5:00 asubuhi.

Amon: Si kweli (kisha akakata simu).

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz

Leave A Reply