The House of Favourite Newspapers

Ndoa ni kama serikali, Rais anaishije na waziri mkuu?

0

couple85620250MUNGU ni mwema sana! Ametukutanisha mimi na wewe Jumanne nyingine tuweze kuzungumza mapenzi na maisha katika ukurasa wetu.

Wiki iliyopita tulijifunza kuhusu madhara ya kupata mpenzi wa kulipa kisasi, bila shaka msomaji wangu ulijifunza mambo mengi na ninaamini yatakusaidia kama kweli utaamua kubadilika.

Tukirudi katika mada ya leo, kama inavyojieleza hapo juu; ndoa ni kama serikali. Naamini kila mmoja wetu anatambua namna ambavyo serikali inaundwa. Mfano ni serikali yetu. Mara baada ya wananchi kutumia nafasi yao ya kikatiba ya kumpigia kura rais, kazi ya pili aliyokuwa nayo rais ni kuunda serikali.

Suala la kuunda serikali halikuhitaji tena kura za wananchi. Jukumu hilo anakuwa nalo rais peke yake. Ndiyo maana unaona kila enzi zimekuwa na utawala wake. Alivyotawala Hayati Julius Nyerere ni tofauti na Ali Hassan Mwinyi. Alivyotawala Mwinyi ni tofauti na Benjamin Mkapa. Mkapa  hakufanana kabisa na Dk Jakaya Kikwete, Kikwete naye ni tofauti kabisa na Dk. John Magufuli.

Nimetumia mfano huo ili wewe msomaji wangu uwe karibu na mada yangu. Uchunguzi usio rasmi unaonesha kwamba kumekuwa na ongezeko kubwa sana la kesi za wanandoa. Watu wanaishi kwenye ndoa kwa miezi mitatu, mwaka mmoja au miwili wanaachana.

Moja kati ya sababu kubwa ambazo zinatajwa kusababisha kesi hizo au wanandoa wengi kuachana ni kushindwa kuunda serikali yao. Wanashindwa kuishi maisha yao. Wanalazimisha kuishi maisha ya wengine, wanafeli.

Mke anataka kuishi kitajiri kama ambavyo rafiki yake anaishi na mumewe. Analazimisha maisha ya ghali wakati uwezo huo hawana. Mke anataka kuendeshwa na majirani. Vivyo hivyo kwa mume, naye anaendeshwa na marafiki, ndugu au hata wazazi.

Akipata tatizo, anauliza kwa wazazi au watu waliomzidi umri akiamini kwamba ndiyo sehemu sahihi ya kupata msaada. Bahati mbaya kule anakoomba ushauri nako anakutana na mtu ambaye naye si sahihi, anampotosha na kujikuta akiingia kwenye matatizo zaidi.

Ndiyo maana nikasema ndoa ni kama serikali. Mume ndiyo rais. Mke ni kama waziri mkuu. Ili mume aweze kufanikiwa, anahitaji waziri mkuu makini. Watakayeelewana. Atakayekubali anguko la pamoja. Kukabiliana na changamoto zote, shinda na raha.

Msiendeshwe na mtu. Msiongozwe na wazazi. Msiongozwe na marafiki au jamaa. Undeni serikali yenu. Mnakutana wawili, kila mtu ana tabia zake lakini mnapaswa kuishi kama kitu kimoja. Mvumiliane. Kila mmoja akubali udhaifu wa mwenzake.

Usitoe nje udhaifu wa mwenzako. Ubebe na uufanye kama changamoto yako. Tafuta suluhu au tiba ya changamoto hiyo. Mume mpe kipaumbele mke, vivyo hivyo kwa mke, ampe kipaumbele mumewe.

La mwisho ambalo ni la msingi zaidi, mtangulizeni Mungu katika kila jambo. Muombeni yeye, mtegemeeni na hakika hakuna changamoto mtakayokutana nayo na mkakosa majibu yake!

Tuonane toleo lijalo.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz

Leave A Reply