The House of Favourite Newspapers

Wadau Wahimiza Juu Ya Taarifa Kudumisha Uwekezaji Nishati Safi na Salama Majumbani

0
Mwenyekiti wa TZLPGA, Benoit Araman akizungumza na wageni waalikwa kwenye mjadala huo (hawapo pichani).

Dar es Salaam, 9 Februari 2024: Katika kudumisha jitihada za Serikali kwenye kampeni ya matumizi safi na salama ya gesi za majumbani, Umoja wa Wafanyabiashara wa Gesi (LPG) za Mitungi ya Majumbani nchini (TZLPGA) wamekutana na waandishi wa habari kujadili njia endelevu za kukuza sekta hiyo kupitia uwezeshaji wa taarifa.

Umoja huo ulioanzishwa mwaka 2023 unaundwa na kampuni 6 zinazofanyabiashara ya gesi za mitungi kwa matumizi ya majumbani ambazo ni CAMGAS, O-GAS, LAKE GAS, TAIFA GAS, ORYX GAS, MANJI GAS na PUMA ENERGY.

Akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria mjadala huo, Mkurugenzi Mkuu wa umoja huo, Amos Jackson alinukuliwa, ‘tunaamini kuwa ukusanyaji na usambazaji wa taarifa sahihi kwenye sekta hii utasaidia kuleta mageuzi makubwa kwenye kufanikisha azma ya nchi yetu kupiga hatua kwenye matumizi ya gesi za mitungi majumbani. Kwaio uwepo wenu hapa utasaidia sana kupanua ufahamu wetu kupitia maoni yenu kama wadau muhimu wa sekta hii’.

Mkurugenzi Mkuu wa TZLPGA, Amos Jackson akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani) kwenye mjadala huo.

Amos alinukuliwa kuhusu mikakati iliyowekwa na umoja huo, alisema, ‘tumedhamiria kupanua matumizi ya teknolojia hii ya gesi za majumbani katika kupunguza uzalishaji wa kaboni, kuboresha ufanisi wa nishati, na kurahisisha matumizi mbadala ya nishati safi’.

Aidha, Mwenyekiti wa TZLPGA Benoit Araman alisisitiza kuhusu umuhimu wa kudumisha ushirikiano baina ya wadau wa sekta hiyo na serikali. Alisema, ‘niwajibu wetu kuiunga mkono serikali kuhakikisha tunaleta mapinduzi kwenye sekta hii ya gesi majumbani ili kutokomeza uharibifu wa mazingira unatokokana na matumizi ya mkaa’. Aliendelea, ‘mkaa ni tishio kwa maana huchangia kutengeneza hewa ya kaboni ambayo inachafua mazingira na kuleta mabadiliko hasi ya tabia ya nchi’.

Mdhahalo huo uliohudhuriwa na mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dr. James Andilile ambaye ameunga mkono uzinduzi wa kampeni wa kusambaza taarifa sahihi juu ya matumizi salama ya gesi (LPG) kwa manufaa ya taifa kwa ujumla.

TZLPGA imeahidi kushirikiana na wadau wa sekta hiyo kutoa msukumo wa wawekezaji kutoa pesa kwaajili ya kukuza matumizi ya nishati safi na athari zingine chanya zitakazosaidia kuwa tija kwa sekta ya nishati kwaajili ya maendeleo ya Taifa zima.

Leave A Reply