The House of Favourite Newspapers

Lindi: Wairan 7 Waliokamatwa na Tani ya Madawa ya Kulevya Wafikishwa Kortini

0


Raia saba wa Iran akiwemo nahodha wa boti, Jan Miran (42) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kusafirisha heroin zenye uzito wa kilo 504.36 na Methamphetamine zenye uzito wa kilo 355.

Mbali na Miran, washtakiwa wengine ni Issa Ahmad(30), Amir Kasom (35), Salim Fedhmulhammad (20), Ikbal Mohammad(22), Mustaphar Bakshi (20) na Jawid Mohammadi(19).

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao leo Ijumaa Aprili 30, 2021 na jopo la mawakili wa Serikali waandamizi, Joseph Maugo na Juma Maige mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Maria Bantulayne.

Wakili Maige amedai washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 2/2021.

Kabla ya kusomewa mashtaka yao, hakimu Bantulayne amesema washtakiwa hawatakiwi kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo ya uhujumu uchumi.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

Leave A Reply