The House of Favourite Newspapers

Wakazi Wa Kibiti Watakiwa Kumuombea Rais Dk Samia

0
Mbunge wa Jimbo la Kibiti, Twaha Mpembenue.

Pwani, 25 Februari 2024: Mbunge wa Jimbo la Kibiti, Twaha Mpembenue amewataka wakazi wa jimbo hilo kumwombea Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa mema mengi aliyowafanyia na kulibadilisha kabisa jimbo.

Diwani wa Kibiti, Hamidu Ungando akizungumza na wananchi kwenye ziara hiyo.

 

Mbunge huyo akiwa kwenye ziara ya kusikiliza kero za wananchi wa jimbo hilo amewakumbusha wanachi hao jinsi Dk Samia alivyosaidia kwenye ujenzi wa madarasa ya kisasa kwenye kwenye shule za msingi na serikali, zahanati na ujenzi na ukarabati za ofisi za serikali na Chama cha Mapinduzi, ujenzi wa madaraja mbalimbali ikiwemo daraja la Mwera.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya Kibiti, Nurudini Ugama akiongea na wananchi kwenye ziara hiyo.

Kukamilika kwa daraja hilo imekuwa ni historia mpya ambapo sasa linaunganisha eneo hilo na kisiwa kilichokuwa hakifikiki kwa gari na hata mtembea kwa miguu ilikuwa ni lazima uvushwe kwa mtumbwi wa kulipia lakini sasa hivi kunafikika baada ya kukamilishwa daraja hilo na kurahisisha mawasialino kwa jamii.

Sehemu ya wananchi wakiwa kwenye mkao wa kusikiliza.
Mbunge wa Kibiti, Twaha Ally Mpembenue akiwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Kibiti, Makaoni Hassani Majilo

Mpaka sasa Mbunge huyo ameshatembelea kata zote 16 vijiji 58 na vitongoji 194 kati ya vitongoji 269 kwa ajili ya ziara yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali katika jimbo hilo ambapo kila alipofika umati wa wanachama kutoka vyama vya upinzani wamekuwa wakirudisha kadi za vyama vyao na kuomba kupewa kadi za Chama cha Mapinduzi.  HABARI NA PICHA ZOTE: ISSA MNALLY /GPL

Leave A Reply