The House of Favourite Newspapers

Mtambo wa Kwanza Bwawa la Nyerere Waanza Kuzalisha Umeme, Megawati 235 Zaingizwa Gridi ya Taifa

0

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Mashaka Biteko leo tarehe 25 Februari 2024 ameshuhudia kuwashwa kwa mtambo wa kwanza katika Mradi wa Julius Nyerere na kungiza megawati 235 kwenye Gridi ya Taifa.

Akizungumza mara baada ya zoezi hilo amesema kuwa kuingia kwa megawati 235 kunafanya mgao wa umeme kupungua kwa asilimia 85 nchini.

“Ninafurahi kusema kile ambacho tuliahidi kufikia tarehe 25 Februari tutakuwa tumeingiza umeme wa mtambo namba 9 kimekamilika,” amesema Dkt. Biteko.

Amesema kuwa mtambo namba 8 unatarajiwa kukamilika mwezi Machi na kufanya jumla Megawati 470 kuingia kwenye Gridi ya Taifa.

Ameongeza kuwa kazi ilipaswa kukamilika mwezi wa sita lakini kutokana na msukumo uliowekwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umefanya kazi kukamilika kabla ya wakati.

“Tunamshukuru sana Mhe. Rais kwani wakati anaingia madarakani mradi huu ulikuwa asilimia 33, amefanya kazi kubwa kuhakikisha fedha za Mradi zinapatikana kwa wakati,” amesema Dkt. Biteko.

Kwa upande wake, Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema kuwa pamoja na uwepo wa changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi Serkali itaendeea na jitihada za utunzaji vyanzo vya maji ili kuhakikisha maji kwa ajili ya uzalishaji umeme yanapatikana.

Leave A Reply