The House of Favourite Newspapers

Wakazi Wa Kitongoji Cha Lumnyozi Kibiti Walivyoipa Jina Shule Yao

0

Wakazi wa Kitongoji cha Lumnyozi kilichopo Kibiti mkoani Pwani wikiendi iliyopita walikutana na kufanya mkutano mkubwa wa kupendekeza jina shule iliyojengwa na wananchi hao kwa kushirikiana na jitihada za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dk. Samia Suluhu Hassan ambapo mengi yaliibuka kwenye kikao hicho.

Katika kikao hicho uliibuka mjadala mzito wa kutoa jina la shule hiyo ambayo awali ilikuwa ikiitwa Chifu Angaya ambapo majina mbalimbali yalitolewa pamoja na kutajwa sababu za majina hayo lakini mwisho wa yote waliafikiana iitwe Sekondari ya Lumnyozi.

Kitendo cha kuteua jina hilo kilisababisha mvutano mkali hali iliyosababisha baadhi ya wananchi kushika mabango na kuhamasisha yapitishwe majina waliyopendekeza wao.

Jimbo la Kibiti kwa hivi karibuni limekuwa kwenye hamasha kubwa ya kimaendeleo chini ya Mbunge wa Jimbo hilo, Twaha Mpembenwe na Diwani wa Viti Maalum maarufu kama Mama Chitanda au Mama Maendeleo ambao mpaka sasa wamefanya mambo makubwa sana haswa katika sekta ya elimu, afya miundombinu, utatuzi wa migogoro na mengineyo.

Kinamama wa Kibiti wakiwa makini kwenye mkutano huo.

 

Mmoja wa wazee wa kijiji akizungumza kwenye mkutano huo.

 

Kinamama wa Kibiti na wakiwa mbele katika suala la elimu. 

Wanakijiji na mabango yao kwenye mkutano huo.

Bango hilo kama linavyosomeka

Mwananchi wa Kijiji cha Lumnyozi akisisitiza jambo.
Leave A Reply