The House of Favourite Newspapers

Uchaguzi Kenya: Nusu Ya Wapiga Kura Wameshiriki Uchaguzi Kenya (Video)

0
Wafula Chebukati

Chebukati: Waliojitokeza kupiga kura ni 48%

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Kenya Wafula Chebukati amesema wanakadiria kwamba idadi ya waliojitokeza kupiga kura leo kufikia wakati wa kufungwa kwa vituo saa kumi na moja jioni ni asilimia 48.

Akihutubia wanahabari, mwenyekiti huyo amesema vituo 87 kati ya vituo vyote vya kupigia kura vilifunguliwa, ambavyo ni vituo 35,564.

Kati ya vituo hivyo, fomu za matokeo kutoka kwa fomu za matokeo kutoka kwa fomu 27,124 zimepokelewa.

“Vituo 5,389 ambavyo vimetapakaa kote nchini havikufunguliwa. Baadhi vimo katika kaunti nne ambazo nilitangaza awali kwamba uchaguzi umeahirishwa,” amesema.

Bw Chebukati amesema vituo kamili vilivyoathiriwa vitatangwa kesho katika gazeti rasmi la serikali.

Baadhi ya watu wameshutumu tarehe mpya ya uchaguzi iliyotangazwa na Bw Chebukati wakisema Jumamosi ni siku ya ibada kwa waumini wa kanisa la Kiadventisti ambao ni wengi katika kaunti ambazo uchaguzi umeahirishwa.

Bw Chebukati hata hivyo amesema walizingatia mambo mengi kabla ya kutangaza tarehe mpya.

“Matokeo ya uchaguzi ni lazima yatangazwe katika siku saba. Lazima tujinyime baadhi ya mambo. Wasiotaka kupiga kura hawatalazimishwa,” amesema.

 

Mtu mmoja auawa mjini Kisumu, ngome ya upinzani

Takriban mtu mmoja ameuawa na wengine watano wamejeruhiwa na polisi kwenye ngome ya upinzani huko Kisumu magharibi mwa Kenya.

Polisi wametumia vitoa machozi na risasi kutawanya waandamanaji ambao wanasusia marudio ya uchaguzi wa urais.

George Odhiambo wa umri wa miaka 19, alipelekwa hospitali kuu ya mji wa Kisumu akitokwa damu nyingi.

Alifariki wakati madaktari walijaribu kukoa maisha yake.

Daktari mmoja katika hospitali hiyo aliiambia BBC kuwa Bw. Odhiambo alipoteza damu nyingi baada ya kupigwa risasi katika mtaa mmoja wa mabanda mjini Kisumu.

Polisi wemekuwa wakikabiliana na waandamanaji mjini Kisumu tangu mapema asubuhi.

Jaji mkuu David Maraga apiga kura

Jaji mkuu nchini Kenya David Maraga alipiga kura yake leo kwenye shule ya msingi ya Bosose kaunti ya Nyamira.

Mwezi Agosti Jaji Maraga aliweka historia pamoja na majaji wenzake watatu kwa kufuta matokeo ya urais.

Jana Jumatano alifika mahakamani peke yake wakati alitangaza kuwa mahakama, haukuwa na uwezo wa kusikiliza kesi iliyokuwa imewasilishwa kwenye mahakana ya juu, kwa sababu hakukuwa na majaji wa kutosha kusikiliza kesi hiyo.

Upigaji kura katika uchaguzi wa urais wa marudio Kenya unafanyika katika  ofisi za ubalozi nchini Tanzania

ambako Wakenya wachache wamejitokeza asubuhi jijini Dar es Salaam na mjini Arusha.

Sehemu ya ubalozi wa Kenya nchini Tanzania ulioko jijini Dar es Salaam.

Faith Wambui Njogu, mmoja wa waliofika kupiga kura ameambia akiongea na BBC amesema ana furaha kwa kutekeleza wajibu wake.

“Nawaambia tu (Wakenya) wapige kura kuwe na amani, cha muhimu amani. Tupendane sote,” amesema.

 

Moto wa matairi ukiendelea kuwaka katika mitaa ya Kisumu.

Katika maeneo mengi ya Kisumu, mji ambao ni ngome ya Raila Odinga, wakazi wamefunga barabara na kuchoma matairi sehemu mbalimbali.

Mwandishi wa BBC Alistair Leithead amesema hajashuhudia kituo chochote ambapo upigaji kura unaendelea.

Ametutumia picha hii:

Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee akiongea jambo baada ya kupiga kura.

Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee amepiga kura yake katika eneo la Mutomo, Gatundu katika kaunti ya Kiambu.  Amesema amefurahi kwamba raia wanajitokeza kupiga kura.

“Tumechoshwa na uchaguzi na sasa ni wakati wa kusonga mbele. Uchaguzi ni fursa kwa raia kuwachagua viongozi kama ilivyosema Mahakama ya Juu. Hebu tuwachague viongozi na tusonge mbele,” amesema.

 

Kenyatta na Odinga.

WANANCHI wa Kenya wanatarajia kushiriki katika uchaguzi wa rais leo huku hali ya utulivu ikiendelea kushuhudiwa katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki baada ya kukamilika kwa kampeni za uchaguzi. Taarifa iliyotolewa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) inasema  maandalizi ya uchaguzi huo yamekamilika huku vyombo vya usalama vya Kenya vikitangaza kwamba vimejiandaa kikamilifu kusimamia zoezi la uchaguzi huo ili lifanyike kwa amani.

Karatasi ya kupigia kura yenye majina ya wagombea.

“Vituo vya kupiga kura vitafunguliwa kuanzia saa 12 asubuhi kesho (leo) na Rais Uhuru Kenyatta atapiga kura kwenye Shule ya Msingi Mutomo iliyoko Gatundu South, Kiambu. Shule hiyo imeelezwa kukarabatiwa siku chache zilizopita ili iwe na muonekano mzuri na kwa heshima ya kiongozi huyo,” imesema IEBC.

Raia akipiga kura.

Mpinzani mkuu wa Uhuru, Raila Odinga anayegombea kupitia muungano wa vyama vya upinzani (NASA), alijiandikisha kupiga kura kwenye eneo la Kibera, jijini Nairobi japokuwa ameshatangaza kujitoa. Mshindi wa kiti cha urais anapaswa kupata asilimia 50+1 ya kura. Uchaguzi wa mara hii nchini Kenya unatajwa kuwa na ushindani mkubwa huku kukiwa na wasiwasi wa kuibuka machafuko katika baadhi ya maeneo na kuna taarifa kuwa baadhi ya watu wameyahama makazi yao wakihofia usalama wa maisha yao.

CREDIT: BBC SWAHILI NA KTN NEWS

VIDEO: UCHAGUZI KENYA

Leave A Reply