The House of Favourite Newspapers

Wakina Mama wa Korogwe Wafurahia Mafunzo ya Ujasiliamali ya Vodacom

0

001 Meneja Ruzuku wa Vodacom  Tanzania Foundation Sandra Oswald(wapili kushoto) akipatiwa maelekezo na Mariam Jecha (wapili kulia)ambaye ni  bibi  masoko wa kikundi cha 2 Seeds  kilichopo kijiji cha  Tabora Wilaya ya Korogwe Tanga , juu ya utengenezaji na upakiaji wa viazi na mihogo vinavyozalishwa na kikundi hicho  baada ya kupata mafunzo  ya ujasiliamali toka taasisi isiyo ya kiserikali ya 2Seeds  ya nchini Marekani  yenye makazi yake makuu Wilayani humo, Mradi huo inafadhiliwa na Vodacom Tanzania Foundation,wengine kwenye picha ni wajumbe wakikundi hicho.

002Meneja Ruzuku wa Vodacom  Tanzania Foundation, Sandra Oswald (kulia) akishirikiana na wanakikundi cha 2Seeds, wa  kijiji cha  Tabora Wilaya ya Korogwe Tanga  kumenye viazi  kwa ajili ya kutengenza Clips  wakati alipotembelea kikundi hicho kukagua maendeleo ya miradi  mbalimbali ya ujasiliamali ,ufugaji, Kilimo iliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania Foundation kwa  kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la 2Seeds Network  la nchini Marekani  na kufanya kazi zake nchini ambapo  makazi yake makuu  yapo Wilayani Korogwe.

004Meneja Ruzuku wa Vodacom  Tanzania Foundation, Sandra Oswald ( kushoto) akisisitiza jambo kuhusiana na  jiko la kisasa la  kukaingia viazi la kikundi cha 2Seeds kilichopo kijiji cha Tabora Korogwe ,wakati alipotembelea kikundi hicho kukagua miradi mbalimbali ya ujasiliamali inayofadhiliwa na  Vodacom Tanzania Foundation kwa  kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la 2Seeds Network  lililopo nchini Marekani.  

006Mariam Jeche na Mwenyekiti  Asha Rajab  wa  kikundi cha 2Seeds kilichopo kijiji cha Tabora Korogwe Tanga, wakimuonyesha mbogambaoga na embe zilizokaushwa  kwenye mashini ya jua  iliyotengenezwa kitalaam Meneja Ruzuku wa Vodacom  Tanzania Foundation, Sandra Oswald (kushoto)wakati alipotembelea kikundi hicho kukagua maendeleo ya  vikundi Vinne  vilivyodhaminiwa na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya kupatiwa elimu ya ujasiriamali ,ufugaji,kilimo  kwa kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la 2Seeds Network  la nchini Marekani.

003

Mwenyekiti wa kikundi cha 2Seeds kilichopo kijiji cha Tabora Korogwe Tanga,Asha Rajab akimuonyesha Meneja Ruzuku wa Vodacom  Tanzania Foundation, Sandra Oswald ( kushoto) moja ya mifuko yenye embe iliyotengenezwa kitalaam, tayari kwa kupelekwa sokoni, kwa mauzo. Kikundi hicho ni miongoni mwa vikundi Vinne  vilivyopata elimu ya ujasiriamali ,ufugaji,kilimo  kwa ufadhili wa Vodacom Tanzania Foundation  kwa  ushirikiano na shirika lisilo la Kiserikali la 2Seeds Network  la nchini Marekani  na kufanya kazi zake nchini. 

005

Mwenyekiti wa kikundi cha 2Seeds kilichopo kijiji cha Tabora Korogwe Tanga,Asha Rajab (Kulia)akimuonyesha Meneja Ruzuku wa Vodacom  Tanzania Foundation, Sandra Oswald ( kushoto) moja ya mashine ya jua inayotumika kukaushia  embe,na mbogamboga   iliyotengenezwa kitalaam,  wakati alipotembelea kikundi hicho kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali ya ujasiriamali,Iliyofadhiliwa na Vodacom Tanzania Foundation  kwa  ushirikiano na shirika lisilo la Kiserikali la 2Seeds Network  la nchini Marekani. 

Leave A Reply