The House of Favourite Newspapers

24 Wafariki kwa Tetemeko Uturuki

0

WATU 24 wamefariki kwa tetemeko la ardhi lililotokea jana  huku wengine takriban 804 wakijeruhiwa.

 

Rais Recep Tayyip Erdogan amesema kati ya waliojeruhiwa, watano wamefanyiwa upasuaji na wanane wapo kitengo cha wagonjwa mahututi.

 

Aidha, tetemeko hilo lililokuwa na ukubwa wa kipimo cha Richter 7.0, limeikumba Ugiriki na kusababisha vifo vya vijana wawili ambao waliangukiwa na ukuta katika ukanda wa Bahari ya Aegean  na kuharibu miundombinu katika miji ya Pwani.

 

Watu katika mji uliopo magharibi mwa Uturuki, wa Izmir wamekusanyika katika mitaa baada ya kuyakimbia majengo yao wakitafuta usalama. Meya wa mji huo amethibitisha kuwa takribani majengo 20 yameharibiwa.

 

Taarifa zilizotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Suleyman Soylu, kupitia mtandao wa Twitter zimesema  miji mingine iliyoharibiwa na tetemeko hilo ni Bornova na Bayrakli.

 

Aidha, Waziri Soylu ameongeza kuwa uchunguzi bado unaendelea katika eneo hilo.

Leave A Reply