The House of Favourite Newspapers

Waliofariki Ukanda Gaza Wafikia 132

0

IDADI ya watu waliouawa kwa mashambulizi Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza imefikia 132, ambapo 32 kati yao ni watoto na 21 ni wanawake, huku Israel ikipoteza watu tisa tangu mapigano kuanza siku ya Jumatatu.

 

Siku ya Jumamosi (Mei 15), madaktari katika Ukanda wa Gaza walisema watu saba walikuwa wameuawa kufuatia mashambulizi ya anga ya jeshi la Israel katika eneo la kaskazini la Ukanda huo.

 

Wakazi wa huko waliripoti pia taarifa za jeshi la wanamaji la Israel kurusha makombora kutokea Bahari ya Mediterenia.

 

Katika mitaa ya Ukingo wa Magharibi, wanajeshi wa Israel waliwauwa waandamanaji saba wa Kipalestina siku ya Ijumaa (Mei 14), wakati ghasia zikizuka katika maeneo mbalimbali ya Israel, ambako raia wa Kiyahudi na Kiarabu wanapambana.

 

Milio ya ving’ora vya tahadhari ilisikika kwenye miji mikubwa miwili ya kusini mwa Israel asubuhi ya Jumamosi, baada ya Hamas kurusha makombora mengine kutokea Gaza.

 

Tangu  mapigano kuanza siku ya Jumatatu, zaidi ya makombora 2,000 yamesharushwa kutokea Gaza kuelekea Israel, yakiwauwa watu tisa, mmoja mtoto mdogo na mwanajeshi mmoja na kujeruhi watu 560.

 

Leave A Reply