The House of Favourite Newspapers

Wallace Karia minne Tena

0

WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wamemthibitisha Wallace Karia kuwa Rais wa TFF kwa kipindi kingine cha miaka minne.Hayo yalijiri jana Jumamosi katika Mkutano Mkuu wa TFF uliofanyika Tanga, ukienda sambamba na Uchaguzi Mkuu wa TFF ambapo Karia alikuwa peke yake kwenye kinyang’anyiro cha kuwania urais.

 

Karia anaiongoza tena TFF kwa kipindi cha miaka minne baada ya awali kuingia madarakani Agosti 2017.Karia baada ya kupitisha kwa kishindo akipata kura za ndio 80 za wajumbe wote, alimteua Athumani Nyamlani kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF.

 

Baada ya zoezi la kumpitisha Karia, Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF wakaanza kupiga kura kuchagua Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF ambapo Kanda ya Kwanza, mshindi ni Lameck Nyambaya aliyepata kura 40, akiwashinda Athumani Kambi (kura 6) na Osea Lugano (kura 35).

 

Kanda ya 2, mshindi aliibuka Khalid Abdallah Mohamed aliyepata kura 55 akimzidi Zakayo Mjema mwenye kura 26.Kanda ya 3, James Mhagama alipata kura 46 na kuwa mshindi akiwazidi Abuu Sufian Silia (kura 27) na Mohamed Mashandu (kura 8).

 

Kanda ya 4, Mohamed Eden alipata kura 52 na kuwa mshindi, akifuatiwa na Osuli Kusuli aliyepata kura 20 na Hamis Juma Kitila kura 8.Kanda ya 5, Vedastus Lufano alishinda kwa kura 35, akifuatiwa na Salum Umande Chama (kura 32) na Salum Kulunge (kura 14).

 

Kanda ya 6, mshindi ni Issa Mrisho Bukuku mwenye kura 58, akifuatiwa na Kenneth Pesambili aliyepata kura 11 sawa na Bras Kihondo.Wakati huohuo, Karia alipendekeza wajumbe wanne ambao ni Athumani Nyamlani kutoka Dar, Ahmed Mgoi (Kigoma), Hawa Mniga (Dar) na Said Sud (Tanga).

NA ISSA LIPONDA NA DENIS CHAMBI, TANGA

Leave A Reply