The House of Favourite Newspapers

Nabi Aanza na Makambo, Mayele

0

KOCHA Mkuu wa Yanga, raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi, amepunguza muda wa mapumziko wa washambuliaji wake Wakongomani, Heritier Makambo na Fiston Mayele.


Hiyo ikiwa ni siku chache
tangu watoke kusaini na kuomba ruhusa ya kurejea nyumbani kwao Kinshasa, Congo kwa ajili ya mapumziko na kumaliza matatizo.

 

Nyota hao wawili walisaini mikataba yao juzi kwa kila mmoja kusaini miaka miwili baada ya kufikia muafaka mzuri na mabosi wa Yanga.

 

Mmoja wa mabosi wa Yanga, ameliambia Championi Ijumaa, wachezaji hao juzi usiku walisafiri kuelekea Congo kwa ajili ya kukamilisha matatizo ya kifamilia kabla ya kurejea tena.

Bosi huyo alisema kuwa washambuliaji hao waliomba ruhusa ya wiki mbili ambazo kocha huyo amezikataa huku akiwapa wiki moja pekee.Aliongeza kuwa lengo la kuwakatalia washambuliaji hao ni ili waiwahi kambi ya timu iliyopangwa kuwa nchini Morocco.

 

“Siku chache baada ya kusaini mikataba ya kazi ndani ya Yanga, Makambo na Mayele jana (juzi) usiku waliondoka nchini kurudi kwao kujiweka sawa tayari kwa kazi.

 

Makambo alitua nchini hivi karibuni bila begi lolote ili kuja kukamilisha dili lake, lakini jana (juzi) viongozi wa Yanga walieleza anakwenda kuoa lakini kocha Nabi amempa wiki moja pekee.

 

“Washambuliaji hao wote walisafiri pamoja kuelekea Congo kwa ajili ya kumaliza matatizo ya kifamilia,”alisema bosi huyo.

 

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa alizungumzia hilo kwa kusema: “Ni kweli washambuliaji hao wamerudi nyumbani kwao kwa ajili ya kumaliza matatizo ya kifamilia lakini watarejea nchini haraka.”

Stori: Wilbert Molandi, Dar es Salaam

Leave A Reply