The House of Favourite Newspapers

Wamarekani Wamwaga Fursa za Tehama Bongo – Video

0

 

Kampuni ya Merita Technologies Ltd ya Marekani yenye uzoefu kwenye masuala ya Teknolojia ya Mawasiliano kwa zaidi ya miaka 30 imefungua tawi lake nchini na inatarajia kuanza kutoa mafunzo kwa vijana wenye hamu ya kujifunza masuala mbalimbali yahusuyo Tehama kuanzia Septemba mwaka huu.

 

Uzinduzi wa Merita Technology nchini Tanzania, umefanyika katika makao yake makuu, Masaki jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi na baadhi ya vijana wanaojishughulisha na masuala mbalimbali ya teknolojia.

 

Abena James, Mkurugenzi Mtendaji wa Meritas Technologies amesema lengo la kampuni hiyo, ni kuwajengea vijana wa Kitanzania uwezo na kukuza maarifa yao katika maeneo mbalimbali ikiwemo kutengeneza programu za kompyuta (SOFTWARE DEVELOPMENT).

 

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Abena amefafanua masuala mbalimbali kuhusu kampuni hiyo na jinsi vijana wa Kitanzania watakavyonufaika na mafunzo hayo yatakayokuwa yanatolewa na jopo la wataalam waliobobea kwenye masuala ya Teknolojia ya Mawasiliano (Tehama) na kueleza kuwa hii ni fursa muhimu kwa vijana wa Kitanzania kujiandikisha na kuhudhuria katika mafunzo kwani yatabadilisha maisha yao.

 

Ndani ya Kampuni ya Merita, kumesheheni wataalam wenye uzoefu mkubwa katika Teknolojia ya Mawasiliano. Miongoni mwao, ni Muta ambaye kwa zaidi ya miaka ishirini, amekuwa akifanya kazi nchini Marekani, akishiriki pia katika miradi kadhaa mikubwa kutoka kwa makampuni makubwa, na hapa anaeleza jinsi alivyo na shauku kubwa ya kuwafundisha vijana wa Kitanzania, ili nao waweze kupata ujuzi na maarifa ya kutosha, kupitia Merita Technology Tawi la Tanzania.

 

Kwabena, ni miongoni mwa waasisi wa Kampuni ya Merita, akiwa na uzoefu na ujuzi mkubwa katika masuala mbalimbali yahusuyo teknolojia ya mawasiliano. Katika uzinduzi huo, naye alipata nafasi ya kuzungumza, na hiki ndicho alichokisema:

 

Kazi imebaki kwako ewe kijana wa Kitanzania! Je, unataka kutimiza ndoto zako za kuwa bingwa wa masuala ya teknolojia ya mawasiliano Tehama? Unataka kuwa mtaalamu wa kutengeneza software? Tembelea website yao kwa kubofya www.meritatech.com kwa maelezo zaidi au unaweza kupiga simu namba 0676 339 971.

 

Leave A Reply