The House of Favourite Newspapers

Askofu Ruwai’chi: Naagiza Mapadri Wote Dar Lazima Mkachanjwe, Tuache Utoto

0
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Yuda Tadheus Ruwai’chi amewaagiza mapadre wote wa jimbo hilo kupata chanjo ya ugonjwa wa Corona .
Askofu Ruwa’ichi ametoa wito huo leo Jumanne, tarehe 24 Agosti 2021, katika Kituo cha Hija cha Pugu, jijini Dar es Salaam, wakati akihubiri kwenye adhimisho la misa takatifu ya mazishi ya Padri Paul Peter Haule.

Padri Haule aliyefariki dunia tarehe 18 Agosti 2021, kwenye Hospitali ya Kardinali Rugambwa, Ukonga, akipatiwa matibabu. Alikuwa Paroko Msaidizi wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Petro, Oysterbay mkoani Dar es Salaam.

 

“Tulimuomba Mungu ajaalie kupatikana kwa chanjo sasa imepatikana badala ya kutumika watu wameingia katika malumbano ya kusema haya na yale dhidi ya chanjo. Kipindi tete. Ajabu tumeanza malumbano. Tutumie fursa tunitunze na kujihami.

 

“Nawahimza yafuatayo, zingatieni maagizo ya wataalamu wa afya. Tieni bidii ya kuyafanyia kazi. Tusingojee hadi mambo haya yatutinge, tutumie vizuri fursa alizotupa Mungu kujikinga na kujihami na kwa sababu hiyo, sijui ni mapdri wangapi ambao mmeshachanjwa, lakini leo naomba nitoe agizo.

 

“Kila padre akachanjwe, kila padre akachanjwe, tusifanye utoto na mzaha, tusifanye lelemama, hii uviko 19 haina mjomba na shemeji na inatuondolea uhai, wale wanaopiga kelele, achaneni nao! Yawekeni pembeni. Tujihami. Na tuendelee kumwomba Mungu atunusuru na hili janga!”” amesema Ruwai’chi.

 

“Nawaalika wenye umri wa kustahili kuchanjwa mkachanjwe. Najua kuna maneno mengi, lakini Baba Mtakatifu Francis katangulia kuchanja, nami nimewapa mfano nimekuwa wa kwanza kuchanja,” amesema Askofu Ruwa’ichi na kuwaomba Watanzania wafuate ushauri unaotolewa na wataalamu wa afya, kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

Leave A Reply