The House of Favourite Newspapers

Wanafunzi 393 Wafutiwa Matokeo Mtihani Darasa la Saba

0

BARAZA la Mitihani Tanzania (Necta) limewafutia matokeo watahiniwa 393 waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani ya kuhitimu darasa la saba 2021.

 

Akitangaza matokeo hayo leo Jumamosi Oktoba 30, 2021 Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema baraza limezishauri mamlaka husika kuwachukulia hatua waliohusika na udanganyifu huo.

 

“ Baraza limezishauri mamla kuwachukulia hatua wale wote waliohusika kwa namna moja au nyingine kusababisha kutokea kwa udanganyifu katika mitihani” amesema Dk Msonde.

 

Msonde amesema pia baraza limezuia kutoa matokeo ya watahiniwa 128 ambao waliugua au kupata matatizo na kushindwa kufanya mtihani kwa masomo yote au baadhi ya masomo.

 

Amesema watahiniwa hao wamepewa fursa nyingine ya kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa mujibu wa kifungu 32(1) cha kanuni za mitihani.

 

Kutazama Matokeo Darasa la Saba 2021 <<Bofya Hapa>>

Leave A Reply