The House of Favourite Newspapers

Gigy Money Anunua Ugomvi wa Kiba na Shilole

0

Jambo linazidi kuwa jambo kwani lile bifu la kukata na shoka la wasanii wa Bongo Fleva, King Kiba na Shilole limepata wafuasi wengi na sasa limenunuliwa rasmi na mwanamama Gigy Money.

 

Katika ugomvi huo, Kiba alidai kuwa hakumualika Shilole kwenye uzinduzi wa albam yake ya Only One King uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar, wiki mbili zilizopita.

 

Kwa upande wake, Shilole anasema alialikwa tena kwa kadi maalum na alipostiwa kwenye ukurasa wa Instagram wa King Kiba na kwamba hata akiwa ukumbini, jamaa huyo alimshukuru kwa sapoti yake.

 

Katikati ya mkanganyiko huo, Gigy ameibuka na kutangaza kuwa upande wa Shilole na kwamba haogopi chochote kitakachompata.

Cc; @sifaelpaul

Leave A Reply