The House of Favourite Newspapers

Wanafunzi, Wafanyakazi UDSM Waliofariki Ajalini Waagwa – Video

Miili ya miili ya wafanyakazi na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) waliofariki kwa ajali baada ya gari la wagonjwa walilokuwemo, kugongana na lori, imeagwa katika ukumbi wa Nkrumah wa chuo hicho.

Mhariri Mwandamizi wa Global Publishers, Elvan Stambul (wa pili kulia) akiaga miili ya marehemu.

Ajali hiyo ilitokea katika maeneo ya Ubungo River Side jijini Dar es Salaam majira ya saa 2 usiku wakati gari hilo likipeleka mgonjwa kutoka Mabibo Hostels kwenda katika Hospitali ya UDSM.

Mary Soko enzi za uhai wake.

Waliofariki dunia kwa ajali hiyo ni, Maria Godian Soko (mwaka wa kwanza COSS) na Steven E Sango (CPE CoET mwaka wa pili), dereva James na nesi wa Chuo hicho.

 

VIDEO: FUATILIA TUKIO HILO

Comments are closed.