The House of Favourite Newspapers

Wanafunzi Wanne UDOM Wafariki Ajalini

0

Wanafunzi wanne wa Chuo Kikuu Dodoma (Udom) wamefariki dunia katika ajali ya basi la kampuni ya Machame iliyotokea Machi 30, 2021 mkoani Manyara. Wanafunzi waliofariki katika ajali hiyo ni Queen Mollel, Mwamvita Jumanne, Leogard John na Glory Godlisten.

 

 

Akizungumza na Mwananchi Digital jana Ijumaa Aprili 2, 2021 makamu mkuu wa chuo hicho, Profesa Faustine Karran Bee amesema vifo hivyo ni simanzi kwa chuo hicho.

 

 

Amesema wanafunzi hao huwa na ratiba ya kurudi nyumbani baada ya kufunga chuo, walipenda kuungana na familia zao kusherehekea sikukuu ya Pasaka.

 

 

“Jana tumetuma wawakilishi katika maeneo ambayo mazishi yao yanaendelea, napenda kutoa pole kwa familia na Taifa kwa msiba huu kwani wanafunzi ndio kwanza walikuwa wamemaliza chuo na kwa hakika walikuwa tegemeo la kuleta mabadiliko kwenye familia zao,” amesema.

 

 

Ofisa habari wa chuo hicho, Beatrice Mtenga amesema chuo kilifungwa Machi 27, 2021 kwa muda wa wiki mbili, hivyo wanafunzi wengi hupenda kutumia likizo kwenda kuonana na familia zao.

 

 

Ahmad Abdulrahman ambaye ni mwanafunzi wa chuo hicho anayesoma shahada ya sanaa na elimu amesema, “ nimeguswa sana na msiba huu mzito, kwetu umetuathiri sana kwani wapo baadhi yao ni rafiki zangu na tulikuwa tukishauriana mambo mengi ya elimu.”

 

 

Ajali hiyo ilitokea kijiji cha Kiongozi Wilaya ya Babati mkoani Manyara.

Leave A Reply