The House of Favourite Newspapers

Wanajeshi 14 Watanzania Wauawa DR Congo

Umoja wa Mataifa umethibitisha kuwa takribani wanajeshi 14 kutoka Tanzania waliokuwa wanalinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo (DRC) wameuawa na wengine 53 kujeruhiwa vibaya baada ya kambi yao kuvamiwa na waasi mapema leo.

 

Taarifa ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kupitia mtando wa Twitter imeeleza.

“Taarifa za awali katika eneo la shambulio mjini Kivu Kaskazini zinaonesha kuwa takribani walinda amani 12 kutoka Tanzania wameuawa na wengine 44 kujeruhiwa vibaya.“amesema Guterres.

Bw. Guterres amesema shambulio hilo ndilo mbaya zaidi kuwahi kutekelezwa dhidi ya walinda amani wa UN katika historia yake miaka ya karibuni huku akielezwa kusikitishwa na tukio hilo.

“Ningependa kueleza kusikitishwa kwangu na shambulio hilo lililotekelezwa usiku wa jana dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRC.

Shambulio hilo lilitekelezwa Alhamisi jioni kwenye kambi ya jeshi ya Semuliki eneo la Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

 

Taarifa ya Umoja wa Mataifa imesema wanajeshi 5 wa jeshi la DR Congo (FARDC) waliuawa pia kwenye shambulio hilo.

“Natuma salamu zangu za rambirambi kwa jamaa na marafiki wa wanajeshi wa kulinda Amani na wanajeshi wa FARDCwaliouawa au kujeruhiwa,” amesema mwakilishi mkuu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DR Congo ambaye ndiye pia mkuu wa kikosi cha walinda amani cha MONUSCO.

 

Kufuatia vifo hivyo tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambi rambi kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt, Hussein Alli Mwinyi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Gen. Vennance Salvatory Mabeyo, Maafisa wote wa Jeshi na kwa familia zote za marehemu.

 

“Nimepokea kwa mshituko mkubwa taarifa za kuuwawa askari wetu kumi na wanne na wengine arobaini na wanne kujeruhiwa na wawili hawajapatikana huko DRC wakati wakitekeleza majukumu ya ulinzi wa amani. Natoa pole sana kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na familia, Wakati tukisubiri taarifa kamili kutoka DRC niwaombe Watanzania tuwe na subira, Mungu wetu yuko pamoja nasi“- Mhe Dkt. John P. Magufuli.

Snura: Faiza Anatafuta Pa Kutokea

Comments are closed.