The House of Favourite Newspapers

Wanakijiji Walia Kubomolewa Nyumba Zao, na Kufukuzwa Kwenye Makazi, Naibu Meya Azungumza

0
Habiba Nguzo akionesha ilipokuwa nyumba yake.

 

 

WAKAZI wa Kijiji cha Mbogo kilichopo Pongwe mkoani Tanga wamelia kubomolewa nyumba zao na kuondolewa kwa nguvu eneo hilo  wanalodai kuanza kuishi tangu likiwa pori miaka mingi iliyopita.

Jamaa akichambua vipande vya matofari vilivyosalia.

 

 

Wananchi hao wamedai kuwa sababu ya kuondolewa eneo hilo kimabavu ni unyanyaswaji wanaofanyiwa na mtu mwenye pesa anayejiita mwekezaji aliyemilikishwa eneo hilo.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Saruji, Clever Muhile akizungumza na wanahabari kuhusiana na mgogoro huo.

 

 

Wakitoa kilio chao wananchi hao wamesema baada ya kubomolewa makazi yao ili kumpisha mwekezaji huyo hawajapewa fidia wala sehemu ya kujihifadhi ingawa wamesema kuna wenzao wamepewa fidia pamoja na hifadhi ya muda.

Naibu Meya wa Manispaa wa Tanga, Joseph Joseph Colivas alipokuwa akizungumza na wanahabari kuhusiana na tukio hilo.

 

 

Kutokana na kukosa hifadhi wananchi hao wamedai kuishi kwa kutangatanga huku wengine wakijibanza vichakani na kuwaomba viongozi wa ngazi za juu kuliangalia upya suala hilo na kuwatetea maana suala limeshafika kwa viongozi mbalimbali lakini bado haki yao haijapatikana.

Martin Albeto (mwenye kofia) na wanakijiji wenzake wakitafakari jambo huku wakiangalia makabuli ya ndugu zake ambayo amesema hajui hatayaachaje naye kuondoka.

 

 

Miongoni mwa wanakijiji waliodai kukumbwa na mkasa huo ni pamoja na Habiba Seif, Abdallah Kindamba, Yohana Cleopa, Mariam Twaha, Zainab Stambuli, Hamida Nguzo na Martin Albeto.

Wanakijiji hao wakiwa wamepumzika eneo hilo baada ya nyumba zao kuvunjwa.

 

 

Baada ya kuzungumza na wakazi hao wanahabari wetu walimtafuta Mwenyekiti wa Mtaa wa Saruji lilipo eneo hilo, Clever Muhile ambaye alisema anaufahamu mgogoro huo na anavyojua tayari ulishamalizika.

 

“Ndugu mwandishi mimi mwenyewe nilikuwa mkazi wa eneo hilo lenye mgogoro ambalo historia yake lilikuwa shamba la Amboni lakini ilipofika mwaka 1996 kampuni hiyo ilifilisika ndipo wafanyakazi wake wakawaruhusiwa kulima mazao ya muda na wasipande vitu vya kudumu hapo ndipo wavamizi walipoanza kuingia eneo hilo”.

 

“Licha ya uvamizi huo lakini ukweli ni kwamba eneo hilo lilishapata mwekezaji na ana nyaraka zote za umiliki na kwakuwa umefika wakati analitaka eneo lake haina budi kulitumia hapo ndipo wale waliovamia wakaanza kugoma kutoka ndiyo chanzo cha huo mgogoro”, alimaliza kusema mwenyekiti huyo.

 

“Baada ya kuzungumza na mwenyekiti huyo wanahabari wetu walikwenda mpaka kwa diwani wa kata hiyo ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Tanga, Joseph Colivas ambaye naye alilitolea ufafanuzi sakata hilo.

 

 

“Mimi hilo sakata nalifahamu sana na tumekaa vikao mbalimbali kulisuruhisha, hao wananchi hilo eneo wamelivamia wakati likiwa na mwekezaji mwenye hati nalo.

 

 

“Hiyo kesi ilipoanza mwekezaji akataka kuwatoa bila fidia lakini mkuu wetu wa mkoa alimuomba huyo mwekezaji atumie busara kwa kuwalipa fidia ambapo mwekezaji huyo alitii jambo hilo kwa asilimia themanini.

 

 

“Aliwapa wanakijiji pesa taslimu pamoja na viwanja ili wakaanzishe makazi mapya lakini wengine waliugomea utaratibu huo na kuzidi kuukoleza mgogoro huo,” Hayo ndiyo yaliyopo ndugu waandishi. Alimaliza kusema Meya huyo.

Leave A Reply