The House of Favourite Newspapers

Wanamuziki Dansi wampiga tafu Makonda

0

RC Makonda (2)WANAMUZIKI wa Dansi nchini Jumamosi hii (leo) wanatarajia kuungana na  kufanya tamasha kubwa na la aina yake ambalo linategemewa kuwa gumzo litakalofanyika katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar.

Tamasha hilo ambalo limeandaliwa na Tanzania Band Festival, lina malengo ya kumsapoti Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika kampeni yake ya kuchangia madawati mashuleni kwani sehemu ya mapato ya tamasha hilo yatakuwa kwa ajili ya kampeni hiyo.

“Tumeamua kushirikiana ili kumsapoti mkuu wetu wa mkoa Makonda kwa namna anavyojitolea katika kuwasaidia wanafunzi lakini hata yeye amekuwa akiusapoti Muziki wa Dansi,” alisema Said Mfaume mratibu mkuu wa tamasha hilo.

Katika tamasha hilo  kutakuwa na bendi kumi zitakazoshiriki ambazo ni  Msondo Ngoma,Sikinde, Mapacha wa Tatu,Yamoto Band, Banana Zorro,Tip Top,Syklight, FM Academia na nyingine nyingi huku kiingilio kikiwa shilingi 15,000 tu.

Leave A Reply