The House of Favourite Newspapers

Bill Nas azidi kuteswa na madawa ya kulevya

0

BILNAS BILLNAS CHAFU POZI GREGORY ALLSTARTZ DAR MULTITECH ZONEMSANII anayefanya vizuri kwa sasa kwenye Tasnia ya Muziki wa Hip Hop, Bongo Bill Nas hivi karibuni amefunguka kuwa sakata la kumhusisha yeye na utumiaji wa madawa ya kulevya linamtesa sana kutokana na ukweli kuwa hajihusishi nayo lakini zaidi ni namna anavyopata wakati mgumu kuwaaminisha watu kuwa hahusiki.

Akistorisha na BBM, Bill Nas alisema kuwa Watanzania wanatakiwa kufahamu kuwa yeye ni mtu mwenye elimu ambaye hayuko tayari kupoteza muelekeo wa maisha yake kisa kikiwa madawa ya kulevya.

“Suala la kunihusisha na matumizi ya dawa za kulevya linanitesa sana kwa sababu situmii na inanilazimu kutumia nguvu kubwa kulikanusha, ninaomba watu wafahamu siwezi kuharibu maisha yangu kisa madawa ya kulevya,” alisema Bill Nas.

Leave A Reply