The House of Favourite Newspapers

Wananchi Buchosa Wafanya Ibada Kumuombea Magufuli

0

WAKATI taifa likiwa katika kipindi Cha maombolezo ya Hayati Dkt. John Magufuli, wananchi wa Jimbo la Buchosa wamekusanyika na kufanya maombi maalumu ya Kumuombea Hayati Magufuli katika uwanja wa Nyehunge.

Aidha, wananchi hao walipata wasaa wa kusaini katika kitabu cha kumbukumbu cha maombolezo ya hayati Dkt. Magufuli kilichokuwepo katika ibada hiyo.

Baadhi ya wananchi walioshiriki ibada hiyo wamemweleza Hayati Magufuli kuwa alikuwa ni mpenda watu hasa watu wa hali ya chini kutokana na kuwapigania haki zao.

Abdallah Hussein mkazi wa Nyehunge amesema atamkumbuka Hayati Magufuli kwa utekelezaji wa ahadi zake alizokuwa akitoa katika kipindi chake cha uongozi wake.

Pia Hussein anaamini viongozi ambao amewaacha watatekeleza ahadi za Hayati Magufuli hususani ujenzi wa barabara ya Sengerema kwenda Nyehunge kwa kiwango cha lami kama alivyokuwa ameahidi kipindi cha kampeni na hiyo itakuwa njia nzuri ya kumuenzi Rais Magufuli.

Joyce John mkazi wa Nyakarilo amewaomba Watanzania kuungana na kushirikiana kuendeleza maendeleo ambayo ameyaacha Hayati Magufuli huku akisisitiza kumuunga mkono Rais Mpya Mhe.Samia Suluhu Hassan ili aweze kuleta maendeleo.

 

Leave A Reply