The House of Favourite Newspapers

Ben Pol: Magufuli Alikuwa Rais Wa Kweli

0

WAKATI nchi ikiwa kwenye majonzi mazito ya kumpoteza Rais wake, Dk John Pombe Magufuli ‘JPM’ baadhi ya mastaa ndani na nje ya Bongo wameendelea kumlilia kwa staili tofauti zinazowaongezea maumivu mashabiki wao.

 

Kwa upande wake, staa wa muziki wa RnB Bongo, Benard Paul ‘Ben Pol’ amesema anaumia mno kwani anajua Rais Magufuli ni mtu mwenye msimamo wa kweli.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA mara baada ya kutokea kwa msiba huo juzi, Ben Pol anasema kuwa, Magufuli alikuwa ni mtu ambaye anapenda kunyoosha mambo na kama kitu hakiwezekani, anasema hadharani kuwa hakiwezekani na kama kinawezekana, basi anahakikisha kinafanyika kwa wakati.

 

“Kiukweli tumepoteza mtu mmoja makini sana, tumempoteza Rais wa wanyonge na shujaa wa Afrika nzima kwa jumla, kitu kimoja ambacho nitakikumbuka sana kutoka kwake ni msimamo wake, yaani kama kitu kinawezekana, basi atahakikisha kinafanyika muda huohuo, tena kwa usahihi, lakini ndiyo hivyo, Mungu amempenda zaidi, tunamuombea apumzike kwa amani,” anasema Ben Pol akiungana na mastaa wenzake kumlilia JPM.

STORI: MEMORISE RICHARD, DAR

Leave A Reply