The House of Favourite Newspapers

Wananchi Wazua Timbwili Kituo Cha Polisi, RPC Asimulia Tukio-Video

0

Wananchi wa kata ya Galula wilayani Songwe Mkoani Songwe wamezingira kituo cha polisi ili kulishinikiza jeshi la Polisi Mkoani hapa kuyaachia mabegi ya tunguli za waganga wa kienyeji walizokamata katika msako wa kutokomeza wapiga ramli chonganishi.

 

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani hapa Janeth Magomi amesema kuwa.

 

Alipokea taarifa kutoka kwa mkuu wa kituo Cha polisi Galula kuwa Wananchi walizingira kituo hicho baada ya kukamata mabegi yenye tunguli ili kulishinikiza jeshi la polisi kuyaachia mabegi hayo na kumshinikiza Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji kurejesha fedha walizokuwa wamechangishana kwa lengo la kuwaita waganga hao.

 

Wananchi hao walivamia kituo wakiwa na mawe fimbo na mapanga na kuleta taharuki iliyopelekea polisi kutumia nguvu kuwatawanya.

 

Katika hali hiyo watu watatu walijeruhiwa na na wengine 29 walikamatwa na watafikishwa mahakamani ili sheria ichukuwe mkondo wake.

Leave A Reply