The House of Favourite Newspapers

Wanawake kuonyesha kazi za mikono yao Julai 18

0

22 33 44 55

Mandalizi yakiendelea  eneo la maonesho hayo.

Tanzania Gasby Trust inatarajia kufanya maonyesho makubwa ya bidhaa za kazi za mikono za wanawake wajasiriamali wa Dar hivi karibuni.

Maonyesho hayo yatafanyika kuanzia Julai, 18 hadi Julai, 21 mwaka huu kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 12 jioni kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Lengo la maonyesho hayo ni kuhamasisha Watanzania kuwa wazalendo na wenye kupenda kutumia bidhaa za ndani ambazo zina ubora kama zilivyo bidhaa zingine.

Hata hivyo wananchi wanaomba kuhudhuria maonyesho hayo ili kuwaunga mkono wanawake wajasiriamali nchini.

Na Mwandishi wetu.

Leave A Reply