The House of Favourite Newspapers

Wanigeria Waipa Yanga Ubingwa Wa Afrika Baada Ya Kutinga Nusu Fainali

0

YANGA imepewa nafasi ya kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na hata kutwaa ubingwa na Rivers United.

Hii ni baada ya kutinga nusu fainali ya michuano hiyo hivi karibuni baada ya kuiondoa Rivers United kwa jumla ya mabao 2-0. Na sasa wataenda kuvaana na Marumo Gallants ya Afrika Kusini.

Msumari huo wa kuwa Yanga wana nafasi ya kuchukua Kombe la Shirikisho Afrika, umepigiliwa na kiungo fundi wa Rivers United, Fortune Omoniwari, ambaye kwa mdomo wake amesema Yanga watacheza fainali na kuwa hata mabingwa.

“Wanacheza vizuri sana, wana ubora wa kuweza kucheza na timu yoyote na kuweza kupata ushindi wakiwa kwenye uwanja wowote, kwetu haikuwa rahisi kupambana nao kwa dakika 180, walikuwa bora kwenye kila dakika.

“Mpira wa Tanzania unakua kwa kasi, timu zake zinacheza kwa ubora na daraja la juu sana, siyo ajabu kuona Yanga wakifika fainali na kuchukua kombe, wana kila kitu ndani ya uwanja na wanacheza kwa ubora sana ,”aliliambia Spoti Xtra.

Kauli hiyo ya Omoniwar, haikutofautiana na ile ya kocha wake wa Rivers United Stanley Eguma ambaye naye alikiri kuwa Yanga ni noma na hawabahatishi na wanaweza kufanya makubwa zaidi msimu huu.

Yanga watacheza mchezo wa kwanza Mei 10 jijini Dar na Marumo Gallants ya Afrika Kusini baada ya ushindi wa jumla wa mabao 2-0 dhidi ya Rivers, huku Marumo wao wakifika hatua hiyo baada ya kuwatoa Pyramidis FC ya Misri kwa jumla ya mabao 2-1.

Stori: Issa Liponda

ZAHORO MATELEPHONE AFUNGUKA JINSI ALIVYOFILISIKA, AMPIGIA SALUTI MAYELE, URAFIKI WAKE na MWIJAKU…

Leave A Reply