The House of Favourite Newspapers

Simba Yaipiga Mkwara Azam Hatua ya Nusu Fainali Kombe la Azam Sports Federation

0

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa unahitaji ushindi kwenye mchezo wao wa Hatua ya Nusu Fainali Kombe la Azam Sports Federation dhidi ya Azam FC utakaopigwa Nangwanda, Mei 6.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira imetoka kufungushiwa virago na Wydad Casablanca kwenye hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika kwa penalti 4-3 baada ya matokeo ya jumla kuwa 1-1.

Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally alisema kuwa wanatambua wengi hawajapenda matokeo hayo lakini imeshatokea kikubwa ni kusonga mbele.

“Wachezaji wetu walijitoa na kupambana lakini ukatili wa matokeo ya mpira umetufanya tuishie robo fainali. Tunarejea kwenye michuano ya ndani na focus (matazamio), yetu kushinda mechi zetu na Kombe la Shirikisho tunataka kushinda dhidi ya Azam FC.

“Tunajua kwamba ili tuweze kwenda hatua ya fainali lazima tupate matokeo mazuri kwenye mchezo wetu .Bado nafasi ipo na tuna mechi ambazo tunapaswa kucheza wachezaji wetu wanajua umuhimu wa mechi hizo na watapata muda wa kupumzika na kujiandaa kuwakabili wapinzani wetu,” alisema Ally.

Stori: Lunyamadzo Mlyuka

ZAHORO MATELEPHONE AFUNGUKA JINSI ALIVYOFILISIKA, AMPIGIA SALUTI MAYELE, URAFIKI WAKE na MWIJAKU…

Leave A Reply