The House of Favourite Newspapers

Wanne Mbaroni kwa Kukutwa na Meno ya Tembo

0

Jeshi la Polisi mkoani Rukwa limefanikiwa kuwakamata watu wanne wakiwa na Nyara za serikali amabazo ni meno  mawili ya tembo.

 

Jeshi hilo lilipata taarifa kwamba watu wanne wanatafuta wateja wa kununua meno ya tembo Katika Kijiji cha Mtependa na kuweka mtego uliofanikisha kuwakamata watu hao wakiwa kando na eneno la uwanja wa Kanisa la Romani Katoliku walipokuwa wameficha meno hayo.

 

Jeshi la Polisi limesema meno hayo walikiwa wameyafichwa kwenye mfuko wa sanadalusi ambapo thamani yake bado haijajulikana.

 

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Rukwa Kamishina Msaidizi wa Polisi William Mwampaghale amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani punde tu upelelezi ukikamilika.

 

Aidha, ACP Mwampaghale ametoa wito kwa wananchi mkoani Rukwa kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kutoa taarifa za uhalifu ili kuzuia uhalifu.

Leave A Reply