The House of Favourite Newspapers

Wanne Watekwa na Al-Shabaab Kenya

0

Wakandarasi wanne wa Kenya waliokuwa wakifanya kazi zao katika eneo la Wel Garas, kaunti ya Wajir wamearifiwa kutekwa na kundi la watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kikundi cha Al Shabab.

 

Kamishna Msaidizi wa Kaunti ya Wajir Mashariki (DCC) Omar Beja alithibitisha kutokea kwa tukio hilo muda wa saa 10 jioni.

 

Zaidi ya hayo, Bwana Beja alifafanua kuwa watu waliotekwa walikuwa wakifanya shughuli za ujenzi wa barabara kati ya Riba na Konton kabla ya tukio hilo.

 

Aidha, katika tukio hilo inaelezwa kuwa muhuska mmoja kati ya wanne waliotekwa alifanikiwa kuwatoroka watekaji hao baada ya kuwaomba ruhusa ya kwenda kukojoa na kisha kutokomea.

 

“NILIMFANYIA DIAMOND WIMBO BURE, KUHUSU YOUNG D MMH!” – LAMAR

Leave A Reply