The House of Favourite Newspapers

Warembo yawakuta

0

IMG_1132
Gabriel Ng’osha na Makongoro Oging’ RISASI

DAR ES SALAAM: Majanga! Warembo wawili wa viunga tofauti jijini Dar ambao majina yao hayakupatikana wamekutwa na mazito baada ya mmoja kudaiwa kutupwa kutoka kwenye Bajaj kisha kuzimia na kuokotwa huku mwingine akitelekezwa katika kituo cha daladala akiwa hajitambui.

Tukio la mrembo kutupwa kutoka kwenye Bajaj lilijiri hivi karibuni, majira ya alfajiri maeneo ya Kijitonyama-Mpakani B jijini Dar kwenye mtaa maarufu wa Kwamwarabu huku la mrembo wa pili likichukua nafasi majira hayohayo katika Kituo cha Daladala cha Shekilango, Dar.

IMG_1135Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio la awali la mrembo aliyetupwa kutoka kwenye Bajaj, alionekana kuwa amelewa tilalila, jambo lililosababisha baadhi ya wananchi kuhisi ni mmoja wa akina dada wanaofanya biashara haramu ya kujiuza (uchangudoa).

“Itakuwa ametoka kwenye biashara zake, kaamua kukodi Bajaj, akaona hana kitu ndiyo akajirusha maana nilimwona akijirushwa nje na Bajaj kusepa zake,” alisema mmoja wa mashuhuda hao.

Shuhuda mwingine alisema kuwa mrembo huyo hakubakwa kama baadhi ya watu wanavyodhani kwani yeye alishuhudia kila kitu.

IMG_1136“Niliiona Bajaji inakuja mara ilipofika eneo la tukio, huyo mdada aliruka kutoka ndani na kugonga kichwa chini ndiyo maana amevimba nundu juu ya paji la uso kisha Bajaj ilitoka nduki.

“Binti mwenyewe alikuwa amevaa nguo za aibu zilizoacha wazi sehemu kubwa ya mwili wake, akatokea msamaria mwema akamfunika na kanga,” alisema shuhuda huyo aliyeonekana ni mwanamke wa makamo.

IMG_1146Akizungumzia tukio hilo, mwenyekiti wa mtaa huo, Hadija Abbas alisema alipewa taarifa na wananchi kuwa kuna mwanamke ametupwa na anaonekana kama amelewa ila usoni amevimba nundu na hawajui kafanyaje.

Alisema kuwa alipofika eneo la tukio, alimshuhudia binti huyo ndipo akaitaa Polisi wa Kituo cha Kijitonyama ‘Mabatini’ ambao walifika na gari aina ya Toyota Noah kisha kumchukua mrembo huyo kwa matibabu ambapo alipozinduka walimruhusu kwenda nyumbani.

IMG_20160106_081700Katika tukio la mrembo aliyekutwa hoi kwenye Kituo cha Daladala cha Shekilango, awali ilidaiwa kwamba ni mmoja wa wanawake wanaofanya biashara haramu ya ngono maeneo ya Sinza, Dar lakini alipozinduka baadaye, alidai kuwa aligongwa na gari.

Hata hivyo, huku bado akiwa na ‘wenge’, mrembo huyo alisaidiwa na wasamaria wema ambao walimpa huduma ya kwanza kisha kumtafutia usafiri wa kumpeleka nyumbani kwani alidai si mbali na mahali hapo.

Leave A Reply