The House of Favourite Newspapers

Video: Mastaa Watembelea Mjengo wa Mshindi wa Shinda Nyumba

0

 Mastaa Watembelea Shinda Nyumba (1)

Mwandishi wa Global Publishers, Imelda Mtema, akiwakaribisha wasanii mara baada ya kuwasili ndani ya mjengo wa Shinda Nyumba. Kutoka kulia ni Isabela Mpanda, Mama Loraa, Shilole, Amanda, Jini Kabula, Babby Madaha na Flora Mvungi.Mastaa Watembelea Shinda Nyumba (2) Mastaa Watembelea Shinda Nyumba (3) Mastaa Watembelea Shinda Nyumba (4) Mastaa Watembelea Shinda Nyumba (5) Mastaa Watembelea Shinda Nyumba (6) Mastaa Watembelea Shinda Nyumba (7) Mastaa Watembelea Shinda Nyumba (8) Mastaa Watembelea Shinda Nyumba (9) Mastaa Watembelea Shinda Nyumba (10) Mastaa Watembelea Shinda Nyumba (11) Mastaa Watembelea Shinda Nyumba (12) Mastaa Watembelea Shinda Nyumba (13) Mastaa Watembelea Shinda Nyumba (14)

Mastaa Watembelea Shinda Nyumba (15) Mastaa Watembelea Shinda Nyumba (16) Mastaa Watembelea Shinda Nyumba (17) Mastaa Watembelea Shinda Nyumba (18)

Na Mwandishi Wetu

ILE siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na mamilioni ya Watanzania wakitaka kujua ni nani ataibuka mshindi wa shindano la Shinda Nyumba, hatimaye imewadia.

Droo ya shindano hilo ambalo linaendeshwa na Kampuni ya Global Publishers kupita magazeti yake ya Championi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi, Amani pamoja na Uwazi, itafanyika Alhamisi katika Viwanja wa Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi katika droo hiyo, anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda.

Makonda pamoja na mamilioni ya wasomaji wa magazeti ya Global, watapata kumshuhudia mmoja kati ya wasomaji hao akijinyakulia nyumba hiyo ya kisasa kabisa ambayo walikuwa wakiishindania kwa kipindi cha miezi sita kwa kutumia kuponi zilizokuwa kwenye ukurasa wa ndani wa magazeti hayo.

Kabla ya nyumba hiyo haijatolewa kwa mshindi, leo baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya pamoja na wale wa filamu hapa nchini, walifika katika nyumba hiyo iliyopo Salasala nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ili kuishuhudia.

Wasanii hao ni pamoja na Shilole, Baby Madaha, Rashida Wanjara, Isabela Mpanda, Jini Kabula, Mama Rolaa, Flora Mvungi na Mwanaheri.

Baada ya kufika katika nyumba hiyo, wasanii hao walipigwa na butwaa na kushindwa kuyaamini macho yao kwa kile walichokiona.

“Tulifikiri kuwa ni utani, kumbe ni kweli, hakika atakayeshinda nyumba hii atakuwa ameukata kwani ni nyumba nzuri na ya kisasa kabisa.

“Binafsi kama Mungu atakuwa ameniwekea mkono wake natamani niwe mshindi kwani na mimi ni mmoja kati ya wasomaji wa magazeti ya Global tulioshiriki shindano hili,” alisema Jini Kabula.

Kwa upenda wake Shilole, amesema: “Nampongeza sana Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo kwani jambo hili alilolifanya ni la kuigwa na watu wengine.

“Shigongo ameonyesha kuwa ni mtu wa watu kwani amekuwa akifanya biashara yake na watu lakini baada ya kupata faida anarudisha sehemu ya faida hiyo katika jamii, hakika hilo ni jambo la kuigwa na wengine.

“Hata hivyo, ningependa mshindi wa nyumba hii awe mtu wa hali ya chini sana kiuchumi na asiwe mwingine kwani ikiwa hivyo atakuwa amemsaidia mtu ambaye alistahili kusaidiwa, namuomba Mungu iwe hivyo.”

TAZAMA NA USIKIE WALICHOKIZUNGUMZA MASTAA KUHUSU NYUMBA HIYO

Leave A Reply