The House of Favourite Newspapers

Wasanii Mjipange Kwa Mama Samia

0

WASANII wengi wa kike kwenye kurasa zenu mmefurahi taifa kupata rais mwanamke.Mmechekelea sana kumpata, Mama Samia Suluhu Hassan kuongoza usukani wa nchi, hilo ni jema lakini mnajua vilivyo?

 

Mnaweza kusimama mbele yake na kumfurahisha kwa sanaa zenu naye akajumuika nanyi; nawauliza kama unasiri huo mnao?

 

Mnaweza kumfanya awe sehemu ya sanaa yenu kwa kuimba nyimbo za matusi naye akawapa heshima?Mnamhafamu vizuri Mama Samia?

 

Huyu mbali na uchapakazi ni mama wa maadili kwa kiwango cha juu, kuna mtu anabisha kwenye hili?Kama hakuna anayepinga; msanii wa kike unawezaje kuendelea kutafuta umaarufu kwa kuvaa nusu utupu mbele ya rais mstaarabu halafu ukatarajia uungwe mkono; ndiyo maana nimewaambia zama hizi mjipange.

 

Wasanii wa Bongo mnatakiwa kujua Rais Mama Samia ni mtu wa dini aliyelelewa kwenye maadili, msitarajie kumfurahisha kwa nyimbo za ovyo na uvaaji wa ovyo, lazima atakwazika.

 

Katika siku za hivi karibuni kumejitokeza nyimbo na tungo nyingi zilizosheheni matusi, ambazo zinapigwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandaoni.

 

Kama hilo halitoshi siku hizi wasanii wengi wamekuwa hodari kwa kuvaa nusu utupu kana kwamba muziki unahitaji maungo ya siri ndiyo unoge.

 

Ukweli ni kwamba wasanii wanapaswa kuamini kuwa kinachoburudisha ni tungo bora na siyo uvaaji wa tusu utupu na matusi.

 

Wakati nchi ikiwa kwenye mageuzi ya kiuchumi ni jukumu la wasanii wetu nao kufahamu kuwa, wanao wajibu wa kujenga jamii inayoheshimu mila na desturi ambazo zimejengwa kwenye maadili.

 

Usanii wa tungo za matusi na kuonesha maungo nyeti siyo, labda kama wasanii hasa wa kike wanapiga ndege wawili kwa jiwe moja

Leave A Reply