The House of Favourite Newspapers

Penzi La Kajala na Harmonize Bundi Ametua

0

PENZI la Kajala Masanja na msanii Harmonize au Harmo, bundi ametua.Ishu ya kusikitisha ni kwamba wawili hao wameachana kwa aibu nzito.

 

Ubuyu unasema, chanzo cha kapo yao kuvunjika ni kwamba Harmo alitaka “kula kuku na yai lake.” Inashangaza sana.

 

Inasemekana kwamba, jamaa alikuwa akimtongoza mtoto wa Kajala, Paula Paul kwa kumtumia picha chafu.Huku na kule, mtoto akaona “nikizubaa ntaliwa” akaenda kwa mama yake kummwagia ubuyu pwaaaa, kwamba baba wa kambo anataka kunikula!

Yanayosemwa ni mengi; lakini eti ni kwamba mchongo wa kumwaibisha Harmo ulianzia kwa mtu wa karibu na Paula ambaye ni msanii Rayvanny kutoka Lebo ya Wasafi aliyoikimbia Harmo.Kumbuka kuwa Rayvanny na Paula hivi karibuni walizua sintofahamu baada ya kuonekana wakifanya mambo ya kikubwa kwenye video iliyosambazwa, mitandaoni.

 

Sasa habari za chini ya kapeti zinasema, kwamba Rayvanny na Paula bado wako krozi na kwamba wakati mtoto huyo wa kike anatumiwa picha za “kutisha za sirini” na Harmo alikuwa anamfowadia Rayvanny ambaye baadaye akamshauri akiwashe.

 

Mpaka sasa supu ya penzi la Harmo na Kajala imetiwa nazi, Kajala kafuta picha za mpenzi wake huyo aliyejidai naye sana mitandaoni, lakini Harmo kabaki anaogelea aibu kubwa ambayo wengi wameijadili kuwa kama kweli kafanya hivyo basi inawezekana kichwani kulikuwa na “chawa” wanakula akili yake.

 

“Hakika kama ni kweli Harmo kafanya hivyo basi atakuwa na tatizo mahali, maana unawezeje kumwacha mama wa mtoto akiwa tayari kwa mechi kitandani halafu wewe ukimbie kutaka kucheza mchangani utakuwa na ufahamu kweli?” maoni ya mchangiaji mitandaoni.Hata hivyo, wengine wanasema, huwenda ni “kiki ya kisanii” lakini mzee wangu mmoja tunayefanya naye kazi alisema; itakuwa kiki ya kijinga kuliko zote duniani.

HOT POT TOLEO NAMBA 003 | GPL

Leave A Reply