Washindi Benki ya CBA Promosheni ya Weka Amana Wapatikana
WASHINDI wawili wa promosheni ya ‘Weka Amana Ushinde’ kutoka Benki ya CBA leo wamepatikana na kujishindia fedha ambapo mkazi wa Dar es Salaam, Dkt. Julieth Kileo alijishindia kiasi cha Shilingi Milioni moja na kwa upande wa wateja binafsi na wateja wa makampuni alikuwa Astoni Charles aliyeshinda na kupata Sh. Milioni mbili.
Hafla hiyo ya droo ya pili ya promosheni hiyo ilishuhudia kukabidhiwa kwa zawadi hizo kukifanyika jijini Dar es Salaam katika ofisi za benki hiyo.
Washindi wa zawadi hizo walielezea furaha yao kubwa kwa kushinda zawadi na kwamba wataendelea kushiriki huku wakiahidi kuzitumia fedha za zawadi hizo kwa kujiendeleza kimaisha.
NA DENIS MTIMA/GPL