The House of Favourite Newspapers

WASHINDI TUSUA MAISHA NA GLOBAL WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

Pantaleo Asenga, mshindi wa head phones akikabidhiwa zawadi yake na Andrew Carlos, Mhariri wa Gazeti la Ijumaa.

WASHINDI wa droo ya tano na sita wa Shindano la Tusua Maisha na Global inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers chini ya udhamini wa Sokabet, wamekabidhiwa zawadi zao leo, Agosti 10, 2018 katika ofisi za Global Publishers, Sinza Mori jijini Dar es Salaam.

Asenga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) baadhi ya kukabidhiwa zawadi yake.

Waliokabidhiwa zawadi zao ni Emanuel Tenga, mkazi wa Moshi aliyewakilishwa na kaka yake, Elinami Mmari na Erasto Luponela, mkazi wa Makambako waliojinyakulia pikipiki, Catherine Tuli, mkazi wa Mbagala na Augustine Haule, mkazi wa Kinyerezi waliojishindia dinner set.

Catherine Tuli, mshindi wa dinner set akikabidhiwa zawadi yake na Jimmy Haroub, Afisa Masoko wa Global Publishers.

 

Bi Catherine akizungumza na waandishi baada ya kukabidhiwa zawadi yake.

“Tumekabidhi zawadi leo, kwa wale walioshindwa kufika, tumezituma zawadi kwa mawakala wetu wa mikoani ambao watawapigia simu na kuwapa maelezo ya namna ya kubadhiwa zawadi hizo,” alisema Abdallah Mrisho, Meneja wa Kampuni ya Global Publishers.

Elinani Mmari akipokea funguo ya pikipiki kwa niaba ya Emanuel Tenga wa Moshi. Anayemkabidhi ni Saima Seif, Mwakilishi wa Sokabet

Baada ya makabidhiano hayo, washindi wote walipata fursa ya kueleza ya moyoni, na jinsi walivyopokea zawadi zao kwa furaha.

Mmari akizungumza na waandishi baada ya kupokea zawadi kwa niaba ya ndugu yake, Emanuel Tenga.

Wakati washindi hao wakikabidhiwa zawadi zao leo, tayari washindi wengine wa droo ya saba wameshapatikana ambapo msomaji Said Katambo wa Nachingwea, Lindi ameibuka mshindi wa pikipiki mpya.

Erasto Omary, mshindi wa head phones akikabidhiwa zawadi yake na Omary Mdose, Mhariri Msaidizi wa Gazeti la Championi.

Mbali na Said, wengine waliong’ara katika droo ya saba ni Boniface Malick wa Bunju A jijini Dar es Salaam aliyejishindia dinner set, Benard Kasembe wa Pugu Mwakanga aliyejishindia head phones za kisasa za Beats by Dre na Ally Bakari, Mkazi wa Vikindu aliyejishindia jezi mpya.

Augustino Haule akikabidhiwa zawadi yake ya dinner set na Hamida Hassan, Mhariri wa Risasi Jumamosi.

Namna ya kushiriki ni rahisi sana cha kufanya nunua gazeti lako lolote linalochapishwa na Global Publishers kati ya Amani, Ijumaa, Risasi, Ijumaa Wikienda, Championi na Spoti Xtra, kisha funua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya jinsi ya kushiriki. 

Erasto Luponelo wa Makambako, akikabidhiwa funguo ya pikipiki na Ezekiel Kitula, Mhariri wa Gazeti la Championi Jumatatu

 

Itume namba maalum inayoonekana juu ya kuponi hiyo kwa njia ya meseji kwenda namba 0719386533. Hakikisha unahifadhi kiopande cha  kuponi yako  au gazeti lako kwani linahitajika wakati wa kuchukua zawadi.

Mzee Luponelo akizungumza baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya pikipiki
Washindi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa zawadi.
Mzee Luponelo akiijaribu pikipiki yake.

Comments are closed.