The House of Favourite Newspapers

Washindi Wa Magifti Dabodabo Wiki Ya 2 Watangazwa na Kupewa Zawadi Zao

0
Semaji la Kampeni ya Magifti Dabodabo Haji Manara (katikati) akimkabidhi seti ya vifaa vya nyumbani kutoka Kampuni ya Hisense mshindi wa vifaa, Abdul Kilabula kulia ni mkewe Zalubia Magesa na mwanae ambapo naye atakabidhiwa seti yake.

Dar es Salaam, 8 Desemba 2023: Kampeni ya Magifti Dabodabo inayoendeshwa na Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo imeendelea kumwaga neema kwa wananchi ambapo leo washindi 13 wa wiki ya pili wametajwa na kukabidhiwa zawadi zao.

Washindi kutoka ni mikoa mbalimbali ikiwemo Visiwani Zanzibar wamejishindia zawadi mbalimbali ikiwemo mshindi wa milioni moja, milioni tano, milioni kumi na mshindi wa vifaa vya nyumbani kutoka Kampuni Hisense.

Meneja wa Bidhaa za Internet, Eginga Mohamed (kushoto) akizungumza kwenye hafla hiyo. Kulia ni Semaji la Kampeni hiyo, Haji Manara.

Kwa washindi wa jijini Dar es Salaam walifika Makao Makuu ya Tigo jijini na kukabidhiwa zawadi zao na semaji la kampeni hiyo, Haji Manara.

Miongoni mwa washindi waliojitokeza na kukabidhiwa zawadi zao ni Abdul Kilabula mkazi wa Chanika Dar aliyejishindia vifaa vya Hisense ikiwemo friji, Tv ya kisasa na seti ya muziki wa kisasa.

Kama isemavyo kampeni hii ya Magifti Dabobado, Kilabula baada ya kuibuka mshindi aliambiwa aende na ampendae ili naye apewe zawadi hizo ambapo jamaa alienda na mkewe Zalubia Magesa ambaye nae alipatiwa seti kama aliyopewa yeye na kukamilisha dhamira ya Magifti Dabodabo.

Semaji la Kampeni ya Magifti Dabodabo, Haji Manara (kulia) akimkabidhi Emmanuel Mboya mfano wa hundi ya pesa alizojishindia.

Akizungumza na wanahabari Kilabula alisema vifaa hivyo vyote atavitumia na familia yake vingine akiweka kwenye vyumba vya watoto.

Wengine walioondoka na zawadi ni Rehema Said mkazi wa Bunju aliyeondoka na shilingi milioni moja na Emmanuel Mboya ambaye naye amekabidhiwa shilingi milioni moja.

Rehema Said mkazi wa Bunju akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni moja alizojishindia kutoka kwa Semaji la Kampeni hiyo Haji Manara. Kushoto ni Meneja wa Bidhaa za Tigo, Eginga Mohamed.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Meneja wa Bidhaa za Internet, Eginga Mohamed aliyekuwa sambamba na Semaji la Kampeni hiyo aliwashauri watumiaji wa simu za mkononi kutumia mtandao wa Tigo kufanya miamala ya Tigo Pesa, kununua vocha za kukwangua au kwa kutumia Tigo Pesa, kulipa bili na kufanya malipo mbalimbali.   HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS WA GLOBAL PUBLISHERS   

Leave A Reply