The House of Favourite Newspapers

Washindi Wapya wa Vitabu vya Shigongo

0

DROO ya nne ya Promosheni ya Jipatie Kitabu cha Shigongo imefanyika jana ambapo jumla ya washindi wanne wamepatikana na kwa mara ya kwanza washindi wote wametokea nje ya Dar es salaam. Droo ya kupatikana kwa washindi hao ilichezwa na kurushwa Mubashara Global Tv Online.

Washindi hao ni Emmanul Ole wa Shinyanga, Anthony Mavuma wa Mufindi Iringa Mbwana Nyanda wa Morogoro na Simba Timoth wa Simiyu.

 

Washindi watatu walichagua vitabu vya ujasiriamalia ambao ni Emmanuel, Mbwana ba Simba wakati Anthony yeye alitaka kitabu cha hadithi. Washindi wote wamepata maelekezo rahisi kabisa ambayo yatawaweza kujipatia vitabu vyao kwa wakati.

Spoti Xtra na Championi wamekuja na promosheni kabambe kwa wasomaji wake, kupitia magazeti hayo msomaji ataweza kujishindia moja ya vitabu vya mwandishi mahiri Eric Shigongo bure kwa kufuata maelekezo rahisi yaliyopo ndani ya magazeti hayo.

Miongoni mwa vitabu hivyo ni Rais Anampenda Mke Wangu, Kifo ni Haki Yangu, Machozi na Damu na vitabu vya ujasiriamali kimoja kikiandikwa kwa lugha ya Kiswahili na kila droo inatoa washindi watano.

Issa Liponda

Leave A Reply