The House of Favourite Newspapers

Wastara: Penzi tamu nililipata kwa Sajuki tu!

0

WASTARA2G.jpgStaa wa filamu za Bongo, Wastara Juma.

NASEMA ukweli kabisa! Staa wa ‘grade one’ kunako filamu za Bongo, Wastara Juma ameweka wazi kuwa, tangu azaliwe, penzi pekee alilowahi kulifurahia ni la aliyekuwa mumewe na msanii mwenzake, marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’.

WASTARASAJUKIEnzi hizo, Wastara Juma akiwa na aliyekuwa mumewe na msanii mwenzake, marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’.

Akichonga na Amani juzi, Wastara alifunguka kuwa, Sajuki ndiye mtu pekee aliyekuwa akimwelewa na kumpa mapenzi ya dhati.

Aliongeza kuwa, Sajuki ndiye mwanaume aliyekuwa akimlinda siku zote na kumtetea katika jambo ambalo alikuwa akionewa.

“Jamani penzi lililowahi kunipa raha na kunifanya nifurahie maisha ni la Sajuki tu na si mwanaume mwingine yeyote. Hicho ndicho kitu kinachonifanya nimkumbuke sana kila wakati,” alisema Wastara.

Leave A Reply