The House of Favourite Newspapers

Wataalam wa Mionzi Wakutana Dar Kubadilishana Ujuzi

0
Naibu Kamishina wa Polisi DCP, Hussein Laisseri akizungumza katika mkutano huo.
Viongozi mbalimbali walioshiriki mkutano huo wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo.

WATAALAM mbalimbali kutoka nchi tisa wamemaliza mafunzo maalum ya siku tano yaliyokuwa yakihusu masuala ya mionzi ambapo idara mbalimbali za vikiosi vya polisi zimeshiriki kupata mbinu mbalimbali za kielimu.
Mafunzo hayo ni ya sita kufanyika katika nchi nyingine ambapo kwa hapa nchini Tanzania ni kwa mara ya kwanza wakishirikiana na US Department of Energy ya Marekani.
Akifunga mafunzo hayo leo jijini Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi DCP, Hussein Laisseri, amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni utayari wa kawaida wa jeshi la polisi na vyombo vya dola kuwa na wataalam wa kutosha kuhusu kubadilishana utaalaam wa masuala ya mionzi .
Naye Mkurugenzi wa Teknolojia wa Nyuklia katika Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Dkt. Filmi Banzi, amezitaja changamoto zilizopo katika masuala ya mionzi kuwa ni uhaba wa vifaa na ukosefu wa wataalam wa kutosha wa masuala ya mionzi ya nyuklia ambapo msaada mkubwa unatoka katika nchi za nje.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply