The House of Favourite Newspapers

WATANZANIA WA MAREKANI WACHANGIA MRADI OFISI ZA WALIMU

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza jambo katika hafla hiyo.

...Makonda akikata utepe kuashiria kupokea samani hizo.
Baadhi ya walimu waliohudhuria hafla hiyo.
Makonda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wa shule za msingi na sekondari.
Baadhi ya walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa wamekalia vitu vilivyoingia kutokea Nchini Marekani.
Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria hafla hiyo ya kupokea samani zilizotolewa.
Makamu mwenyekiti anayesimamia mradi huo,  Solomon Urio akizungumza jambo.

 

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  amepokea makontena ishirini kutoka kwa Watanzania waishio Marekani yakiwa na vifaa mbalimbali vya samani za ofisi za walimu wa mkoa huo.

 

Akizungumza katika hafla hiyo, Makonda amewashukuru Watanzania hao waishio ughaibuni kwa msaada huo na kuahidi kuwa vifaa hivyo vitatumika kama ilivyokusudiwa.

 

Makonda aliowaomba wadau wa mradi huo wasaidie kulipia gharama za usafirishaji wa samani hizo  na gharama zingine za ndani ili ziweze kupatikana na kutumiwa sehemu husika.  Wakati huohuo, Benki ya Walimu – Mwalimu Commercial Bank – imelipia baadhi ya makontena hayo.

 

Naye makamu mwenyekiti anayesimamia mradi huo,  Solomon Urio, amepongeza juhudi za mkuu huyo wa mkoa  za kutafuta wadau mbalimbali wa kuchangia shughuli za kimaendeleo.

 

NA DENIS MTIMA/GPL

Comments are closed.