Wateja wa Airtel Money Waendelea Kujishindia Mkwanja na Tesa Kimilionea Wiki Ijayo Gari

KAMPUNI ya Airtel leo imeendelea kurudisha fadhila kwa wateja wake kwa kugawa mkwanja kupitia promosheni yake ya Tesa Kimilionea.
Miongoni mwa washindi hao ni mkulima kutoka Chalinze, Pwani, Mashaka Mashaka aliyeondoka na milioni moja na Wakala wa Airtel Money, Nikodemus Nyamocha wa Mbezi Africana Dar, naye ameondoka na milioni moja huku washindi wengine 100 nao wameondoka na mkwanja wao kila mmoja.

Akizungumza baada ya kutangazwa washindi hao, Meneja wa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando amesema lengo la promosheni hiyo ni kuendeleza uhusiano mwema na kubadilisha maisha ya wateja wao waaminifu.
Mmbando ameendelea kusema kuwa droo inayofuata wiki ijayo mshindi mmoja atajinyakulia gari aina ya Toyota IST, mshindi wa pili ataondokana kitita cha milioni 10 na wengine wataondoka na laki moja kila mmoja.
“Droo tutakayochezesha wiki ijayo mshindi wa kwanza atajishindia gari aina ya Toyota IST mwingine milioni 10 na wengine wataondoka na laki moja kila mmoja.
“Lengo letu kuu ni kuboresha maisha ya wateja wetu na kuzidi kuimarisha uhusiano mwema na wateja wetu.

“Hivyo basi tunawaomba na wateja wetu Airtel na watumiaji wengine wa simu za mkononi kutumia mtandao wa Airtel na kufanya miamala mbalimbali kwa kutumia huduma za Airtel Money” alisema Mmbando.
Naye Meja Chapa wa Airtel Money, Gillian Rugumamu ameendelea kuwasisitiza watumiaji wa simu za mkononi kutumia mtandao wa Airtel ili waweze kupata huduma za Airtel Money na kuweza kujishindia mkwanja kupitia promosheni ya Tesa Kimilionea.
Gillian amesema kwa watumiaji wa Airtel unachotakiwa ni kupiga *150*60# na kufanya miamala mbalimbali ndipo unakuwa umeingia kwenye droo hiyo na kuweza kujishindia.