The House of Favourite Newspapers

Wateja wa Tigo Kilolo Kuhudumiwa Kwa Kasi zaidi ya 3G

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, Philemon Namwenga  (wa tatu kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mnara mpya wenye uwezo wa 3G katika kijiji cha Idete, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja wa Tigo kanda ya Kusini, Abbas Abdulrahman, na wa kwanza kulia ni diwani wa viti maalum kata ya Idete, Elina Kivegele, akifuatiwa  na Meneja Mauzo wa Tigo Iringa, Samwel Chanai.

…Wakibadilishana mawazo  baada ya uzinduzi.

…Wakisalimiana na baadhi ya wananchi wa Idete waliofika katika uzinduzi huo.

KAMPUNI  ya mawasiliano ya simu, Tigo, leo imezindua mnara wa 3G katika kata ya Kidete, mkoani Iringa ikiwa moja ya jitihada zake za kufikisha huduma bora za kupiga na kupokea simu, intaneti na kutuma na kupokea pesa kwa wateja wake. 
Akizungumza katika uzinduzi huo katika kata ya Idete, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kilolo, Aloyce Kwezi, aliwakaribisha na kuwashukuru Tigo kwa kuongeza ufanisi wa mnara huo kutoka teknolojia ya 2G hadi 3G.
“Serikali ya Tanzania imefanya suala la viwanda kuwa ajenda yake kuu. Na sisi kama serikali tunatambua umuhimu wa mawasiliano katika kufanikisha hii dira. Tunapenda kuwashukuru sana kwa kuifikiria Kilolo na wananchi wake, maana sekta hii ya mawasiliano ni chachu kubwa sana katika ukuaji na ubunifu wa viwanda mbalimbali,” alisema Kwezi.
Kwa upande wake, Meneja wa Tigo Kanda ya Kusini, Abbas Abdulrahman, alisema  kipaumbele cha Tigo ni kuhakikisha wateja wake wanapata huduma za kisasa za kiteknolojia za simu kama ya 3G.
“Uzinduzi wa leo unaofanyika Kilolo ni mwanzo wa kampeni ya nchi nzima ambapo kutakuwa na uzinduzi wa minara 52 kutoka Tigo itakayozinduliwa kutoka kanda ya Ziwa, Kaskazini, Pwani na Kusini,” alisema.  
Uzinduzi wa minara uaenda sambamba na ofa maalum ambapo wateja watahudumiwa na minara ambayo imeongezewa uwezo kutoka 2G hadi 3G,  watazawadiwa kiasi cha MB 100 za data kila mara watakaponunua kifurushi chochote cha intaneti.
Pia wateja katika maeneo ya minara ya 4G itakayozinduliwa, watazawadiwa  GB 4 za data bure pale wanapobadilisha laini zao za simu kuingia 4G.
“Kuongeza ubora wa mnara huu kutoka 2G kwenda 3G ina maana kwamba wateja wetu wa Kilolo sasa wataweza kupata huduma rahisi na kasi zaidi. Kwa mfano, 3G itaweza kuwapatia huduma ya intaneti iliyo bora ambayo itafungua jamii zilizopo vijijini kuweza kupata huduma za kielektroniki katika nyanja za kibiashara, afya, elimu na serikali ambazo walishindwa kupata huko nyuma. Jambo hili litabadilisha namna watu watakavyojifunza na kufanya biashara,” alisema Abdulrahman. 
 
Alisisitiza kuhusu kazi ambayo Tigo inafanya kuwezesha sera ya TEHAMA ya taifa na kuunga jitihada ya serikali katika viwanda kwa kupanua na kuboresha wigo wa mtandao ili kuwezesha nchi kufaidika katika nyanja mbalimbali za kijamii kama uchumi na elimu kupitia mfumo wa kidijitali. 
 
Minara mengine ambayo imeboreshwa na zitazinduliwa hivi karibuni katika Kanda ya Kusini ukiondoa Kilolo, inapatikana katika maeneo ya Sumbawanga, Katavi, Mufindi, Njombe, Songwe, Mbeya and Songea.
 

Comments are closed.