The House of Favourite Newspapers

Watoto 136 Watekwa Shuleni

0

MAOFISA wa Serikali katika Jimbo la Kaskakazini mwa Nigeria, wamethibisha kutekwa nyara kwa watoto 136 na kwamba wameanzisha mawasiliano na watekaji-nyara katika juhudi za kuwakomboa.

 

Watoto hao wa shule miongoni mwao wakiwemo wenye umri wa miaka mitano walitekwa nyara wakiwa shuleni na watu waliokuwa na silaha kwenye Jimbo la Kaskazini mwa Nigeria.

 

Mmiliki wa shule husika ameliambia Shirika la Habari la AP kwamba, watu hao waliokuwa na silaha wakiwa wamepanda pikipiki waliivamia shule yake na kumuua mtu mmoja na pia kuwachukua kwa nguvu walimu watatu.

Hii ni kadhia nyingine katika mfululizo wa watoto kushikiliwa kwa ajili ya kudai pesa nchini Nigeria.

 

Leave A Reply